Kuzama kwa meli ya Venezuela hivi karibuni, kunasisitiza umuhimu wa kuwa na njia mpya: IOM na UNHCR 

26 Aprili 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM na lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Geneva, Uswisi, wamesikitishwa na vifo vya watu wawili wakati boti ilipozama katika baharí Venezuela Alhamisi ya Aprili 22.

Kwa mujibu wa mamlaka mashinani karibu watu 24 ikiwemo watoto inadaiwa walikuwa kwenye boti wakielekea Carribea kwenye visiwa vya Trinidad na Tobago. Watu saba waliokolewa na boti za Venezuela na miili miwili hadi sasa imepatikana wakati operesheni za uokozi za kusaka manusura wengine 15 wavenezuela ambao bado hawajulikani waliko.  

Taarifa hiyo imewanukuu wawakilishi wa IOM na UNHCR wakisema, “maji ya carribea yanaendelea kupokonya maisha ya wavenezuela. “wakati hali nchini Venezuela inaendelea kuwa mbaya huku janga la COVID-19 likifanya hali kuwa mbaya zaidi watu wanaendelea kuchukua safari hizo hatarishi.” 

Hili ni tukio la hivi karibuni kati ya matukio  kadhaa vinavyohusisha kupinduka kwa boti zilizobeba wakimbizi na wahamiaji wa Venezuela kuelekea visiwa vya Karibea. 

Pamoja na mipaka ya ardhi na baharini ikiwa bado imefungwa kuzuia maambukizi ya COVID-19, safari hizi hufanyika hasa kupitia njia zisizo za kawaida, ikiongeza hatari na hatari za kiafya na ulinzi. 

"Kuzama kwa meli, vifo wakati wa kuvuka mpaka na mateso zaidi vinaepukika, lakini ikiwa tu hatua za haraka na za pamoja za kimataifa zitahamasishwa kupata suluhisho za kiutendaji ambazo zinaweka kuokoa maisha na kulinda haki za binadamu mbele ya majibu yoyote. Kuanzishwa kwa njia za kawaida na zilizi salama, pamoja na kupitia viza za kibinadamu na kuungana tena kwa familia, na vile vile utekelezaji wa mifumo ya nyeti ya ulinzi na mifumo ya kutosha ya mapokezi, inaweza kuzuia utumiaji wa njia zisizo za kawaida, magendo na usafirishaji haramu." Ameongeza Stein. 

UNHCR na IOM wameeleza tena utayari wao wa kutoa msaada na utaalam wa kiufundi katika kutafuta suluhisho za kiutendaji kutoa njia za kawaida ambazo pia huzingatia hatua za kuzuia za COVID-19. Kuna wakimbizi na wahamiaji Wavenezuela zaidi ya milioni 5 duniani kote, 200,000 kati yao wakikadiriwa kuhifadhia katika visiwa vya Karibea.  

 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter