Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutana na Khamisa mkimbizi anayeisaidia familia yake kupata chakula

Khamisa John Adiand mwenye umri wa miaka 19.
WFP/Belinda Popovska
Khamisa John Adiand mwenye umri wa miaka 19.

Kutana na Khamisa mkimbizi anayeisaidia familia yake kupata chakula

Msaada wa Kibinadamu

Jimbo la White ni nyumbani mwa idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2019 Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP liliwasaidia wakimbiizi 387,000 kote nchini Sudan huku sehemu kubwa ya mchango wa chakula ukitoka shirike la Marekania la USAID. Nusu ya wakimbizi hao ni wanawake. 

 

Wanawake wakiwa wameshikilia kadi zao za kupokea mgao wa chakula.
WFP/Belinda Popovska
Wanawake wakiwa wameshikilia kadi zao za kupokea mgao wa chakula.

WFP inawasaidia wanawake kuwa wenye kufanya maamuzi nyumbani kwa kuwapa kadi za mgano wa chakula kwa majina yao. Hii ni moja ya hadithi hizo.

Mgao wa chakula kutoka kwa WFP ni mwokozi kwa wengi ikiwemo Khamisa.
WFP/Belinda Popovska
Mgao wa chakula kutoka kwa WFP ni mwokozi kwa wengi ikiwemo Khamisa.

Akishikilia kadi ya mgao wa chakula kwa meno yake, Khamisa John Adiand mwenye umri wa miaka 19, anapanga foleni kupata mgao wa mafuta ya kupikia ikiwa ni sehemu ya mgao wake wa kila mwezi kutoka WFP.

Anajificha nyuma ya wanawake wengine ili asionekane. Kadi hiyo ya kupata mgao wa chakula imetobolea mashimo ikiashiria miezi ambayo amechukua chakula kwa ajili ya wazazi na ndugu zake wanne.

Kila Mwezi Khamisa, ambaye ana ndoto ya kuwa daktari siku moja, anatembea kutoka nyumbani kwa familia yake hadi kituo cha kugawa chakula cha WFP katika kambi ya Alagaya jimbo la White Nile. 

Kama mmoja wa wanawake viongozi nyumbani kwao amepewa jukumu la kukusanya mgao wa chakula wa kila mwezi kwa niaba ya familia yake.

WFP katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu imelisha wakimbizi 387,000 nchini Sudan.
WFP/Belinda Popovska
WFP katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka huu imelisha wakimbizi 387,000 nchini Sudan.

 

Licha ya kuwa nyumbani ni nchi jirani umbali wa maili 20 hadi mpakani, Khamisa hakuwa na lingine ila kukubali makao yake mapya ya muda. 

Aliwasili katika kambi ya Alagaya miaka mitano iliyopita akiandamana na wazazi wake na nduguze wakisaka usalama. Akiwa na kumbukumbu na tabasamu Khamisa anaeleza nyumbani alikotoka.

“Ninatoka jamii ya watu wa Shilluk na tunazungumza lugha ya Shilluk. Ninatoka jimbo la Upper Nile. Nyumbani ni karibu lakini nahisi kama ni mbali sana. Ninakumbuka ardhi yenye rutuba na miti mizuri. Ninakumbuka nikicheza densi na marafiki, amani iliyokuwa kabla ya vita kuzuka.”

Jukumu lake la kukusanya chakula kwa niaba ya famiaia yake ni moja ya mipango mikuu wa WFP. Mpango huu unalenga kuwapa motisha wanawake kuwa wamiliki wa kadi za kuwapa uhuru kwa kukusanya chakula.

“Ninapenda kuipikia familia yangu. Wakati nitakuwa daktari nitakuwa na uwezo wa kuipikia familia yangu samaki. Samaki anayepikwa kwa makaa na kuni huwa na ladha nzuri sana."

Anafikiria kidogo na kucheka akisema, “labda sitaweza kupika tena, nitamuajiri mpishi kuipikia familia yangu.”

Khamisa, kaka na dada zake wanaonekana wenye ndoto kubwa, na matumaini ya kurudi nyumbani. “Wakati kutakuwa na amani, nitarudi nyumbani na kuisaidia Sudan Kusini kuboresha huduma zake za afya. Kama daktari, nitasaidia watu wengine sio tu familia yangu.” anaongeza Khamisa

Wanawake wakisubiri mgao wa chakula kwa ajili ya mgao wa mwezi mzima.
WFP/Belinda Popovska
Wanawake wakisubiri mgao wa chakula kwa ajili ya mgao wa mwezi mzima.

Sudan kwa sasa inahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wakiwa ni wakimbizi 850,000 waliolazimika kukimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe

Wengi wametafuta hifadhi katika jimbo la White Nile. Kutokana na mchango wa USAID, WFP inaendelea kuwasaidia wakimbizi hawa na chakula.

Utafiti wa hivi majuzi kati ya Aprili hadi Julai mwaka jana ulionyesha kuwa kati ya wakimbizi 1,085 waliofanyiwa utafiti ulionyesha kwa karibu asilimia 68 walio na kadi za mgao wa chakula ni wanawake.

 

Kwa sasa kuna wakimbizi milioni 1.1 nchini Sudan, wengine kutoka nchi jirani. Kwa wengi wanaovuka mipaka haki ya kimsingi ya kupata chakula kawaida huwa ndio hatua ya kwanza kwa usalama.

 

TAGS: WFP, Sudan Kusini, wakimbizi, mgao wa chakula, USAID