Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji ni chachu ya vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Guterres 

Miji kama mji mkuu wa Korea Kusini Seoul ni watumiaji wakubwa wa nishati
Unsplash/Ethan Brooke
Miji kama mji mkuu wa Korea Kusini Seoul ni watumiaji wakubwa wa nishati

Miji ni chachu ya vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Guterres 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mifano kadhaa ya jinsi miji ambavyo tayari inafanikiwa katika hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi alipozungumza katika mkutano wa Kikundi cha C40 wa kundi la miji mikubwa ya Uongozi dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, kwani katikati ya miji wameathirika zaidi na jangala corona au COVID-29, na viwango vya juu vya vifo na upotevu wa uchumi.  

António Guterres, katika hotuba yake hii leo ameangazia jukumu la miji katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi na jinsi ya kujikwamua kutoka kwenye janga la Covid-19. 

Kundi hilo la C40 la miji mikubwa kwa ajili ya uongozi wa mabadiliko ya tabianchi tayari linajumuisha zaidi ya vituo 90 vya mijini.  

Miongoni mwa miji hiyo ni Lisbon, Curitiba, Rio de Janeiro, Salvador na São Paulo.  

Umuhimu 

Kwa Guterres, miji ni "nguvu nzuri na inayokuwa katika jukwaa la kimataifa." 

Na kulingana na yeye, miji hiyo ilikuwa ni miji ambayo ilipata shida zaidi kutokana na janga hilo la COVID-19, na imekuwa na viwango vya juu vya vifo na maambukizo na upotevu mkubwa wa uchumi, pamoja na kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. 

Katibu Mkuu pia amesisitiza umuhimu wa mabadiliko, akisema kwamba hayawezi kupuuzwa 

Zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote ulimwenguni wanaishi mijini. Kufikia 2050, inakadiriwa kwamba karibu watu saba kati ya 10 wataishi mijini.  

Na zaidi ya asilimia 90% ya ukuaji huu unatarajiwa kutokea katika nchi zinazoendelea. 

Ameongeza kuwa hivi sasa, wakaazi milioni 50 wa mijini tayari wanapata athari za kuongezeka kwa kina cha bahari na dhoruba za mara kwa mara au vimbunga vikali. Katikati ya karne hii, zaidi ya wakaazi wa mijini bilioni 3.3 wanaweza kuwa katika hatari ya athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi. 

Hewa ukaa 

Katibu Mkuu amesema miji pia ina alama kubwa ya hewa ukaai, ikitoa asilimia 70% ya gesi chafu ulimwenguni. 

Kwa katibu mkuu, "uwekezaji katika kujikwamua upya na janga la COVIDF-19 ni fursa kwa kizazi hiki kuweka hatua za mabadiliko ya tabianchi, nishati safi na maendeleo endelevu katikati mwa kitovu cha miji, ili kuwaandaa kwa wimbi lisiloepukika la ukuaji wa miji linalokaribia na ambalo halijawahi kutokea." 

Ameongeza kuwa dunia inahitaji kutozalisha kanbisa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050 ikiwa ni kufikia lengo la mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi la kupunguza kuongezeka kwa joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5º C. 

Guterres amesema kuwa muungano unaokua wa nchi, miji, kampuni na taasisi za kifedha umejitolea kufikia lengo hili, lakini akasema kwamba maono haya "hayaonekani katika mipango yao madhubuti." 

Malengo 

Hivyo ameongeza kuwa itakuwa ni lazima kupunguza uchafuzi wa hewa kwa asilimia 45 ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2010 na kuna njia tatu za kufikia lengo hilo: 

Kwanza, amesema kwamba walio kamili wanapaswa kushirikiana na viongozi wa kitaifa kutoa michango kabambe zaidi ya kitaifa, mbele ya mkutano wa wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa au COP-26, ambao unafanyika mnamo Novemba mwaka huu nchini Uingereza. 

Mwaka 2019, meya wa São Paulo, Bruno Covas, alizungumza na UN News juu ya vitendo vya jiji la Brazil vya kupendelea hatua za mabadiliko ya tabianchi. 

Halafu, pili amesema miji inaweza kufanya mipango kabambe ya mkutano ujao na kujitolea kwa kuhakikisha hawazalishi hewa ukaa ifikapo mwaka 2050. 

Na mwishowe, amesema wanaweza kutumia mipangi ya kujikwamua na janga la COVID-19 kuharakisha uwekezaji na utekelezaji katika miundombinu safi, inayojali mazingira na mifumo ya usafirishaji.