IOM na EU wasaidia maelfu ya familia zilizoathiriwa na Nzige wa Jangwani nchini Ethiopia:IOM
IOM na EU wasaidia maelfu ya familia zilizoathiriwa na Nzige wa Jangwani nchini Ethiopia:IOM
“Wakati nzige wa jangwani walipovamia eneo letu kwa ghafla, tulikerwa sana,” anaeleza Galmo Kiyo Waariyo, mkulima anayeishi katika kijiji cha Lafto nchini Ethiopia. “makundi ya nzige yalikuwa makubwa kiasi kwamba yalikuwa yakifunika anga na kuleta giza polepole na muda si muda wananza kutembea kila sehemu.”
Msimu wa kilimo uliopita ulionekana kuleta matumaini mpaka pale nzige wa jangwani walipoanza kuharibu mazao katika eno kubwa la Afrika Mashariki kuanzia mwishoni mwa mwaka 2019 katika kijiji cha Lafto.
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM nzige hao waliwavamia wakati hawakutarajia mnamo Februari 2020, na kuharibu kwa kiasi kikubwa mashamba na malisho yao.
Galmo, mwenye umri wa miaka 58 na mama wa watoto nane, anaishi Dubuluk Woreda eneo la Borena, katika jimbo la Oromia.
Watoto wake watatu ni wa umri wa chini ya miaka mitano; mmoja wa wanafamilia wao ni mgonjwa sana. Yeye ni msimamizi pekee wa familia hiyo.
Katika historia ya familia za kijiji cha Galmo, ni wakulima na wafugaji wanaotegemea mvua.
Kama wengine wengi, jamii yake hupanda mchanganyiko wa mazao, hupanda mahindi kwenye vipande vyao vya ardhi na ufugaji wa kama vile kondoo, mbuzi na kuku, lakini sio wakati wa uvamizi wa nzige.
“Tulijaribu mbinu nyingi kufukuza nzige hao kutoka kwenye mazao na mimea yatu,” Galmo anaendelea kusema na kuongeza kwamba “Tulipiga kelele kwa kutumia sauti zetu na vyombo kama ndoo. Tulikoka moto ili kuleta moshi mweusi kwneye maeneo yenye mimea.”
Vyote hivi havikuwa na mafanyikio katika kuwafukuza nzige hao. “Waliharibu mazao yetu yote, na kutotuacha na chochote mashambani,” amalizia.
“Nilipoteza kila kitu, udongo ukasalia kwenye sehemu iliyokuwa yenye mazao yanayotia matumaini. Bila kutarajia, tulijikuta katika uhaba mkubwa wa chakula amabacho hakiwezi kutusaidia kumudu maisha na wala malisho kwa mifugo yetu.”
Galmo anasema mazao yake yaliharibiwa katika siku tu na pia nyasi na mimea yote iliyokuwa karibu ilisambaratishwa.
Mnamo Februari 2020, mamlaka za serikali zilianza juhudi za kudhibiti nzige hao lakini licha ya uingiliaji wao wa haraka, kiwango chao cha uharibifu kiliacha mazao mengi yakiharibiwa na kuwaacha watu katika mazingira ya kuteseka ikiwemo wale wanaoishi katika kijiji cha Lafto.
Kulingana na shirika la kilimo na chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), nzige wa jangwani ni wadudu waharibufu na wanaohamahama zaidi duniani.
Hua wanakula kila mmmea katika maeneo ya kilimo, na misitu. Hupaa kwa kasi na kuvuka umbali mkubwa.
Kundi moja dogo la nzige kwenye kilomita moja ya mraba wanaweza kula chakula sawa na cha watu 35,000 kwa siku moja.
Ethiopia ilishuhudia uvamizi mkubwa zaidi katika kipindi cha miaka 25. Mnamo 2020, watu milioni 20.2 walikuwa wakikabiliwa na njaa iliokithiri katika kanda ya pembe ya Africa, limesema shirika hilo la FAO.
Ukame wa hivi karibuni na mlipuko wa virusi vya corona au coronavirus">COVID-19 vilikuwa tayari vimeathiri mapato na wafugaji walikuwa wamerejelea kuuza mifugo yao ili kupata fedha za kununua chakula, na kupunguza milo kwa siku.
Kutokana na upungufu wa chakula, jamii zote za wathirika zilikuwa zikiishi kwa kula chochote kitakacholetwa sokoni, na kumaliza kabiza pesa walizokuwa wameweka akiba.
Sasa shirika la IOM kwa msaada wa Euro milioni 2 kutoka shirika la Ulinzi wa raia na kutoa msaasa wa maenedeleo la kamisheni za Haki za Binadamu za Ulaya (ECHO), linazifikia familai zilizoathirika na janga la nzige kwa mfano Dubuluk kwa kuzipatia msaada wa pesa taslimi za kuwawezesha kufikia mahitaji mengi.
“Muungano wa Ulaya umeunga mkono juhudi za kupambana na nazige wa jangwani na madhara yake, sio tu nchini Ethiopia bali pia katika kanda nzima ya Pembe ya Africa. Katika maeneo mengi nzige wamechochea uhaba wa chakula uliokuwepo tayari. Katika ushirikiano na wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo IOM na EU tulichangia Euro milioni 9.5 mwaka 2020 kushughulikia uhaba wa chakula na kutoa msaada wa kuwezesha maisha kwa wafugaji na wakulima walioathiriwa na nzige wa jangwani nchini Ethiopia,” amesema Yassine Gaba, kiongozi wa ofisi ya msaada wa kibinadamu ya Muungano w aUlaya (EU).
Mnamo Oktoba 2020, IOM, katika ushirikiano na serikali na kikosi kazi cha kutoa pesa taslim cha nchi hiyo yani Cash Working Group, walianza kutoa msaada wa pesa taslim kwa familia zilizoathirika zaidi.
Sababu kuu ya hatua hii ilikuwa ni kushughulikia mahitaji ya dharura ya chakula kwa wathirika kulingana na vyakula vilivyowekwa na serikali na pia kuwezesha upatikanaji w amaji, huduma za kujisafi, elimu na malaazi.
Pesa taslim zipatazo ETB 1,500 (karibu sawa na dola za Kimarekani 40) zimetolewa kwa kila familai kwa mwezi katika kipindi cha zaidi ya miezi mine kwa kutumia huduma za kutuma na kupokea fedha. Fedha hizo hutolewa kwa kuzingatia kiwango cha chini zaidi kilichowekwa na kikosi kazi cha kutoa pesa taslimu cha Kmaisheni ya serikali ya kushughulikia majanga (NDRMC) baada ya tathmini ya haraka iliofanywa ili kufuatilia bei ya bidhaa kwa walaji.
Kati ya Oktoba na Novemba 2020, Galmo na kaya zingine katika kijiji chake zilipokea msaada wa ETB 6,000 (saw ana dola 150), na kuwasaidia kutokana na madhara ya uvamizi wa nzige.
Kupitia msaada huu, Galmo aliweza kupata mahitaji ya msingi ya chakula, kununua mbegu, huku akiepuka kuuza mali zake ili apate pesa za kununua bidha.
“Ninafurahi sana kwa msaada wa pesa taslim kama unavyonisaidia sio tu kupata chakula kwa ajili ya familia yangu bali pia kupata tena mbuzi wangu niliokuwa nimeuza. Nimetumia kiasi cha pesa nilizopokea kununua mbegu nzuri nikitaraji kupata mavuno mazuri safari hii,” sasema Galmo.
IOM ilitathimini hali ya soko la walaaji na uwepo wa chakula kwenye soko na mbegu katika maeneo kama West Hararghe, Borena, West Guji, Jerer na Nogob kabla ya kuzindua mradi huo.
Kutokana na haya yote, IOM iliangazia hatari zinazohusiana na ulinzi, jinsia, na uwezekano wa kufikia masoko na vituo vya usambazaji, na pia jinsi wadau mbalimbali kutoka ngazi ya wilaya kushuka chini kwa parokia hadi ngazi ya jamii, walikubali kutumia mifumo ya kielektroniki ya kutuma na kupokea pesa.
Viongozi wa serikali na kijamii walifanya kazi muhimu sana katika kubaini watu wanaositahili kufaidika na mradi huo.
Tangu hatua hii muhimu, izinduliwe Julai 2020, karibu kaya 8,500, au takriban watu 45,000, ambao vyanzo vyao vya mapato viliathiriwa wamefaidika.