Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhaba wa kimataifa wa ubunifu wa dawa za viauvijasumu wachochea kusambaa kwa usugu wa dawa:WHO

Uhaba wa matibabu mapya ya magonjwa makubwa yanayoletwa na bakteria ambayo yamekuwa sugu umewaacha watu katika hatari kubwa ya magonjwa hayo
CDC
Uhaba wa matibabu mapya ya magonjwa makubwa yanayoletwa na bakteria ambayo yamekuwa sugu umewaacha watu katika hatari kubwa ya magonjwa hayo

Uhaba wa kimataifa wa ubunifu wa dawa za viauvijasumu wachochea kusambaa kwa usugu wa dawa:WHO

Afya

Ulimwengu bado unashindwa kutengeneza matibabu mapya ya kupambana na viuatilifu ya ambayo yanahitajika sana, licha ya kuongezeka kwa tishio kubwa na la haraka la usugu wa za vijiuvijasumu au antibiotics, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, iliyotolewa leo . 

WHO inafichua kwamba katika dawa 43 za viuavijasumu ambazo sasa ziko katika matengenezo hivi sasa hakuna hata moja inayoweza kushughulikia vya kutosha shida ya usugu wa dawa katika vijiumbe maradhi hatari zaidi ulimwenguni.
Dk Hanan Balkhy, mkurugenzi mkuu msaidizi wa WHO kuhusu usugu wa dawa au AMR amesema "Kuendelea kushindwa kuzindua, kutengeneza, na kusambaza dawa mpya za kukomesha usugu huo wa dawa kunaongeza  zaidi athari za usugu wa dawa (AMR) na kutishia uwezo wetu wa kutibu magonjwa yayanayosababishwa na vijiumbe maradhi," 
Karibu dawa zote mpya ambazo zimeletwa sokoni katika miongo ya hivi karibuni ni aina za dawa za vijiuavijasumu ambazo ziligunduliwa katika miaka ya 1980.
Athari za AMR ni kali zaidi katika mazingira yenye vikwazo vya rasilimali na miongoni mwa vikundi vilivyo hatarini kama vile watoto wachanga na watoto wadogo. 
WHO inasema homa ya kichomi na maambukizi ya mfumo wa damu ni kati ya sababu kuu za vifo vya watoto wa chini ya umri wa miaka 5. 
Takriban asilimia 30% ya watoto wachanga walipata maambukizi ya hufa kwa sababu ya maambukizo ya vijiumbe maradhi vilivyo sugu dhidi ya dawa za vijiuavijasumu zilizopo. 

Mtaalam wa maabara nchini Bangladesh akijaribu kuchanganya dawa na kifua kikuu sugu (MDRT)
The Global Fund/Thierry Falise
Mtaalam wa maabara nchini Bangladesh akijaribu kuchanganya dawa na kifua kikuu sugu (MDRT)


Matokeo ya Ripoti

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya WHO kuhusu vijiumbemaradhi, hupitia dawa za vijiuavijasumu ambazo ziko katika hatua za kliniki za majaribio na vile vile zilizo katika hatua za awali za matengenezo.
 Lengo ni kutathmini maendeleo na kutambua mapungufu kuhusiana na vitisho vya dharura vya usugu dawa, na kuhamasisha hatua za kuziba mapengo hayo.
Ripoti hiyo inatathmini uwezo wa uwezekano wa dawa za vijiuvijasumu zinazoweza kushughulikia tatizo la usugu zaidi  wa dawa zilizoorodheshwa katika orodha ya kipaumbele cha vijiumbe maradhi sugu ya WHO (WHO PPL).