Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hojaji ya mtumiaji Habari za UN 2021

Nembo
UN
Nembo

Hojaji ya mtumiaji Habari za UN 2021

Masuala ya UM

Karibu kwenye Hojaji ya mtumiaji wa Habari za UNAsante kwa kukubali kushiriki ili tuweze kuboresha vipindi vyetu viweze kukidhi mahitaji yako. Tafadhali fahamu kwamba majibu hayatosema yametumwa na nani na haitokuchukua zaidi ya dakika 4 kumaliza.

Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa kitengo cha habari kimeanda dodoso hili maalum kwa lengo la kupata maoni kutoka kwa watumiaji wa habari zinazoandaliwa kwa lugha 9. Lugha hizo ni Kiswahili, Kiingereza, Kichina, Kirusi, Kifaransa, Kiarabu, Kireno, Kihindi na Kihispania. 

Mathalani ni kwa jinsi gani watu wanaotembelea wavuti za habari zetu wanatumia majukwaa yetu, kipi ambacho kina manufaa zaidi kwenu, kipi kisichowafaa na tufanye nini ili kukidhi mahitaji yao vizuri.

Tunalenga pia kusikia kutoka kwa wale wanaofahamu kuhusu majukwaa mbalimbali ya Habari za UN lakini hawayatumii , ili tuweze kuelewa ni kwa nini  na kwa jinsi gani tunaweza kukidhi mahitaji yao vyema.

Kwa ufupi, hojaji hii itaenda sanjari na maadhimisho ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa wavuti mpya wa Hanari za UN, ikiwa ni wakati mzuri wa kukusanya maoni kutoka kwa wasikilizaji/wasomaji wetu.

Tafadhali bofya hapa ili kujaza hojaji hii na muda hautazidi dakika nne kukamilisha.
Karibu sana