Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Comoro imepokea dozi 12,000 za chanjo ya COVID-19 kupitia COVAX 

Wakomorhi hutembea katika maji ya pwani yenye kina kifupi wakiwa wamebeba vikapu vya mazao ya kilimo vichwani mwao.
UNDP Comoros/James Stapley Wavuvi wakiwa katika shughuliza zao katika visiwa vya Comoro

Comoro imepokea dozi 12,000 za chanjo ya COVID-19 kupitia COVAX 

Afya

Serikali ya visiwa vya Comoro Jumatatu imepokea dozi 12 za chanjo ya Ccorona au COVID-19 aina ya AstraZeneca kupitia mkakati wa Umoja wa Mataifa wa usambazaji wa chanjo COVAX. 

Kwa mujibu wa timu ya Umoja wa Mataifa nchini Comoro inaendelea kuisaidia serikali ya visiwa hivyo vya bahari ya Hindfi na kushirikiana na wadau wengine wa afya katika utoaji wa chanjo hiyo muhimu. 

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema shehena hii mpya iliyowasili itachangia ongezeko la idadi ya watu wanaolengwa kupatiwa chanjo, wakiwemo wahudumu walio msitari wa mbele, wazee walio na umri wa miaka 60 na zaidi, walio na matatizo ya kiafya ya muda mrefu na watu wa shule. 

Serikali ya Comoro ilizindua rasmi kampeni ya chanjo dhidi ya coronavirus">COVID-19 tarehe 10 Aprili mwezi huu sanjari na kupokea msaada wa kiufundi kutoka shirila la afya WHO na shirika la Umoja la kuhudumia watoto UNICEF