Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde wakati wa Ramadhani tushikamane na wakimbizi:UNHCR

Mtoto mkimbizi akibeba boksi la futari wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
UN
Mtoto mkimbizi akibeba boksi la futari wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Chonde chonde wakati wa Ramadhani tushikamane na wakimbizi:UNHCR

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito wa mshikamano kwa mamilioni ya waakimbizi na wakimbizi wa ndani kote duniani ambao wameathirika vibaya na janga la kimataifa la corona au COVID-19 wakati huu ambapo Waislam kote duniani wakijiandaa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhan.  

Akisistiza hilo Kamisha mkuu wa wawakimbizi Filippo Grandi amesema watu hao waliolazimika kukimbia makwao ni lazima wajumuishwe katika program za kimataifa za chanjo na mipango ya kujikwamua na janga la COVIDS-19.  

Pia ameongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili kushughulikia mahitaji yao ya elimu, afya ya akili, ulinzi wa Watoto na kuzuia na kuchukua hatua dhjidi ya ukatili wa kujinsia unaowakabili.    

Amesema ”Wakati huu wa kutafakari na kuonyesha ukarimu , mshikamano wet una watu waliolazimika kukimbia makwao duniani kote unahitajika kuliko wakati mwingine wowote . Katika dhamira ya mwezi mtukufu wa ramadhan natoa wito wa msadaa na mshikamano zaidi na watu hawa wasiojiweza na walio hatarini.”  

Ameongeza kuwa takriban asilimia 85 ya wakimbizi wote duniani wanahifadhiwa katika nchi za kipatyo cha chini ama cha wastan ambazo sasa zinakabiliwa na changamoto za kifedha na mata nyingi zina mifumo isiyojitosheleza ya afya. 

Na matokeo ya janga la COVID-19 ni kwamba wakimbizi na watu waliotawanywa wamepoteza uwezo wao wa kujikimu kimaisha na kutumbukia kwenye lindio la umasikini na kusababishiwa athari kubwa sana. 

UNHCR inakadiria kwamba wakimbii 3 kati ya w4 kote duniani wanaeweza kufikia nusu tu ya mahitaji yao ya msingu au chini yahapo. 

Hali ambayo imezilazimisha familia nyingi kupunguza matumizi yao ya chakula, wengi hawawezi kulipa kodi ya pango, wametumbukia katika madeni au wamelasimika kuwasitiosha watoto masomo hata katika maeneo ambako shule zimefunguliwa. 

Kwa kuanza kwa mweszi mtukufu wa Ramadhan UNHCR imezindua kampeni ijulikanayo kama “Kila dakika ni muhimu” ambayo ni kampeni ya kimataifa ya kuchangisha fedha. 

Fedha zinapokelewa kama Zaka, sadaka au msaada wowote ambao utaweza kuwapunguzia madhila familia zilizolazimika kufurishwa makwao na kuwa mbaliu na familia zao. 

“Kwa pamoja tunaweza kuwasaidia wakimbizi na wakimbizi wa ndani kuwa na mahala pa kukaa, kupata mlo kwa ajili ya futari na matumaini ya kuwa na mustakabali bora” amesema bwana Grandi.