Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawezaje kumpatia kila mtu chanjo dhidi ya Corona? Changamoto Kuu 5 kwa COVAX 

Watu wazima ni miongoni mwa watu wa kwanza kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 Lima, Peru
© UNICEF/Jose Vilca
Watu wazima ni miongoni mwa watu wa kwanza kupokea chanjo dhidi ya COVID-19 Lima, Peru

Tunawezaje kumpatia kila mtu chanjo dhidi ya Corona? Changamoto Kuu 5 kwa COVAX 

Afya

Lengo la mpango wa kimataifa wa usambazaji chanjo kwa nchi za kipato cha chini na kati, au COVAZ, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa   ni kuona dozi bilioni mbili za chanjo zikiwa zimepatiwa kwa robo ya watu katika nchi maskini zaidi itakapofikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2021. Lakni ni changamoto gani kubwa ambazo zinapaswa kushughulikiwa, ili juhudi hizi za kihistoria za kimataifa zifanyikiwe? 

Lengo la mpango wa kimataifa wa usambazaji chanjo kwa nchi za kipato cha chini na kati, au COVAX, unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa   ni kuona dozi bilioni mbili za chanjo zikiwa zimepatiwa kwa robo ya watu katika nchi maskini zaidi itakapofikia mwishoni mwa mwaka huu wa 2021. Lakni ni changamoto gani kubwa ambazo zinapaswa kushughulikiwa, ili juhudi hizi za kihistoria za kimataifa zifanyikiwe?

Chanjo ni sehemu muhimu ya suluhisho  kutokomeza mlipuko wa ugonjwa wa Corona au COVID-19 ikizingatiwa kuwa tangu mwanzoni mwa mlipuko huu shirika la afya la Umoja wa Mataifa, (WHO) limekuwa likichagiza juhudi za pamoja kuhakikisha kwamba kila mtu, sio tu wanaoishi katika nchi tajiri,  apate kinga ya kutosha dhidi ya virusi hivyo vilivyosambaa kwa kasi duniani.

Kutokana na hoja hii, ulianzishwa mfumo wa kimataifa ya kusimamia chanjo dhidi ya corona au  COVAX , taasisi ya kimataifa pekee inayoshirikiana na serikali na kampuni kuhakikisha kwamba chanjo dhidi ya COVID-19 inapatikana kote duniani  kwa matajiri na maskini.  

Mhudumu wa afya ashika kifaa cha chanjo ya covid-19 aina ya AstraZeneca kutoka kwenye kijisanduku baridi nchini Uganda. 
© UNICEF/Adrian Musinguzi
Mhudumu wa afya ashika kifaa cha chanjo ya covid-19 aina ya AstraZeneca kutoka kwenye kijisanduku baridi nchini Uganda. 

Hapa ni mambo matano muhimu ya  kufahamu changamoto zinazoikabili COVAX, na jinsi ya kuzikabili.

1) Udhibiti wa usafirishaji wa chanjo nje ya nchi: sehemu isiyodhibitiwa?

Mwanzoni mwa mlipuko huu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF lilitayarisha mabomba ya sindano bilioni moja kwenye mabohari nje ya nchi ambazo hutengeneza vifaa hivyo. Hatua hiyo ilikuwa na faida kwa kuwa nchi zinazotengeneza ziliibuka na mbinu za kuongeza bei na kubana usambazaji.

Diane abad-Vergara, Afisa mawasiliano WHO kuhusu COVAX na Chanjo ya COVID-19

Nchi nyingi zaidi ziliweka njia za kudhibiti usafirishaji nje ya nchi wa chanjo hiyo, na kusababisha WHO kuonya dhidi ya “uzawa kwenye chanjo”, kitendo kinachoweza kuchagiza kuhodhi chanjo hizo, kupanda kwa bei na kutoa mwanya wa mlipuko kuenea, vikwazo vya kuudhibiti na mateso ya kibinadamu na kiuchumi.

Upatikanaji wa chanjo kwa wote unahitaji juhudi kabambe za kimataifa kuhusu utengenezaji wa chanjo hiyo.  Kuanzia kwa kemikali zinazohitajika kuitengeneza, hadi kwenye vizuizi vya vichupa na plastiki na mabomba, hadi kwenye sindano.

Kwa sababu hii, marufuku za usafirishaji nje ya nchi zinaweza kukwamisha usambazaji wa chanjo. 
Kutokana na njia nyingi za kudhibiti vizuizi vya usafirishaji au uuzaji nje wa chanjo, nchi maskini nazo zitapata nafasi ya kukinga wananchi wake kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kutengeneza chanjo hiyo wenyewe.
“WHO husaidia nchi katika juhudi zake za kupata na kuendeleza uzalisahji wa chanjo na kwa teknolojia na kujenga uwezo”, asema Diane Abad-Vergara, kiongozi wa mawasiliano wa COVAX, “ingawa ubunifu kama huu kwa mtandao wa nchi zinazotengeneza chanjo, na kuzisaidia kujenga misingi yao ziada — hasa barani Afrika, Asia, na  Amerika ya Kusini  — ambazo zitakuwa muhimu kukidhi mahitaji yanayoendelea ya virutubisho na chanjo za badaye dhidi ya COVID-19. Uamuzi  wa uzalishaji kimataifa ungesaidia nchi maskini kutotegemea misaada kutoka nchi tajiri”.

Nchini Uganda chanjo zinasafirishwa kwa kutumia miguu, boti au piki piki.
© UNICEF/Henry Bongyereirwe
Nchini Uganda chanjo zinasafirishwa kwa kutumia miguu, boti au piki piki.


2) Sio rahisi kupata chanjo kwa wale wote wanaoihitaji 
 

Gian Gandhi, Mratibu wa COVAX kwneye UNICEF Kitengo cha usambazaji.

Wakati nchi zote sehemu ya mpango wa COVAX zina miundombinu inayohitajika kupokea vifaa chanjo kutoka ndegeni hadi kwenye mabohari yenye barafu au majokofu hatua zaidi zinaweza kuwa ngumu.
“Ghana, nchi ya kwanza kupokea dozi za COVAX, imekuwa na sifa nzuri za usambazaji wa dozi hizo”, asema Gian Gandhi, Mratibu wa Kimataifawa UNICEF kuhusu  COVAX, “lakini nchi zingine kama zile zilizotawaliwa na Ufaransa katika ukanda wa Afrika Magharibi zimekabiliwa na kipindi kigumu kupata rasilimali zinazohitajika kutoa dozi na kuzisambaza kwenye ukanda huo hadi kwenye miji na vijiji zinakohitajika. Inamaanisha kwamba kwney nchi nyingi maskini zaidi, dozi nyingi zinasambazwa kwneye miji mikubwa”.

“Tunataka kuhakikisha kwamba hamna mtu hata mmoja anayekosa chanjo hiyo”, amesema Bwana Gandhi, “lakini, katika muda mfupi, uwepo wa dozi nyingi mijini inamaanisha chanjo kwa wahudumu wa afya na wahudumu wnegine wa msitari wa mbele mijini, ambako idadi kubwa ya watu huongeza hatari ya kuambukizwa, inapatiwa kipaumbele”.

3) Ufadhili zaidi unahitajika kusaidia kusambaza huduma ya chanjo katika nchi zilizo maskini zaidi

Njia moja ya kuharakisha utoaji wa chanjo, na usambazaji wake kutoka mabohari ya mijini hadi vijijini ni rahisi zaidi ni kuhakikisha kuna fedha. “Ufadhili ni hoja ya msingi, hata wakati wa kuitikia mlipuko”, amesema Bi. Abad-Vergara. “Ili kuendelea kutoa chanjo katika nchi wanachama 190, COVAX inahitaji angalau dola bilioni 3.2 mnamo mwaka 2021. Haraka, yanapofikiwa malengo ya chanjo hii, inategemea wakati chanjo iapofikishwa kwa watu.”

Michango kutoka mataifa mbalimbali, hasa Muungano wa Ulaya (EU), Uingereza na Marekani imeweka hatua kubwa katika kuziba pengo la ufadhili. Hata hivyo, ufadhili wa usambazaji wa chanjo hizo bado ni tata.
UNICEF inakadiria dola bilioni 2 za ziada zinahitajika kusaidia nchi 92 zilizo maskini zaidi kugharamia vifaa muhimu kama vile majokofu, kuwafundisha wahudumu wa afya, gharama za chanjo, na mafuta ya magari yenye barafu ya usafirishaji wa chanjo, na pia inatoa wito kwa wahisani kutoa dola milioni 510 zilizopo papo hapo kama sehemu ya wito wa msaada wa kibinadamu kukidhi mahitaji ya dharura.

Mongolia ilianzisha chanjo nchini mwake mnamo Machi kwa kutumia chanjo aina ya Pfizer/BioNTech COVID-19 iliotolewa kupitia COVAX
© UNICEF/Khasar Sandag
Mongolia ilianzisha chanjo nchini mwake mnamo Machi kwa kutumia chanjo aina ya Pfizer/BioNTech COVID-19 iliotolewa kupitia COVAX


4) Nchi tajiri zaidi ni lazima zigawe dozi za ziada

COVAX inajikuta katika ushindani na mataifa yanayowasiliana moja kwa moja na kuweka makubaliano na kampuni za kutengeneza dawa na hivyo kuweka shinikizo katika suala la upatikanaji na usambazaji wa chanjo. Wakati huo huo nchi tajiri zinaweza kujikuta na ziada ya dozi za chanjo.

“Tunatoa wito kwa nchi hizi kupatia nchi zingine dozi zao za ziada na pia wawasilaine na COVAX na UNICEF haraka iwezekanavyo”, amesema Bwana Gandhi, “kwa sababu itachukua hatua za kisheria, kiuongozi na kioperesheni kuwaweka wanapohitajika. Kwa sasa hatuoni nchi nyingi tajiri zikiwa tayari kugawa chanjo hizo”.

Akionya kuhusu mwelekeo wa sasa, Bi. Abad-Vergara anasema, “mwelekeo wa sasa wa ‘mimi kwanza’ unasaidia wale wanaoweza kulipa ziada na kughairmu makubwa kifedha na maisha ya watu, lakini ni muhimu kufahamu kwamba mahusiano ya kimataifa yasiathiri usambazaji wa dozi na michango kwa COVAX, hususani kupitia mgao wa  dozi wa chanjo hiyo”.

Mjini  New Delhi nchini India, bango linaloeleza mchezo wa kuigiza ukipuuza uongo kuhusu chanjo ya COVID-19.
© UNICEF/Sujay Reddy
Mjini New Delhi nchini India, bango linaloeleza mchezo wa kuigiza ukipuuza uongo kuhusu chanjo ya COVID-19.


5) Kutoamua kuhusu chanjo: Hoja inayoendelea 

Licha ya ushahidi ya kwamba chanjo hii inaokoa maisha, bado shaka na  hofu ya kuitumia inashudiwa karibu kila nchi na hivyo ni suala linalopaswa kushguhulikiwa kwa uendelevu.
Hali hii imesababishwa na uvumi uliozunguka mlipuko wa COVID-19, iliyokuwa hoja kubwa hata kabla ya kutangazwa kwa mzozo wa kiafya duniani mnamo Mei. Umoja wa Mataifa ulizindua kampeni, inayopinga uongo, na badala yake kusambaza habari sahihi na zinazoaminika. 

“Kupitia mlipuko wote, kumekuwepo habari nyingi zikienea”, asema Bi. Abad-Vergara. "WHO inafanya kazi kudhibiti uvumi huu, na pia kujenga imani kuhusu chanjo hizi na kujadilaina na jamii mbalimbali”.