Katibu Mkuu UN akaribisha hatua ya Marekani kutengua amri yake dhidi ya ICC

5 Aprili 2021

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha hatua ya serikali ya Marekani ya kufuta amri ya kuzuia mali ya baadhi ya watu wanaohusishwa na vizuizi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya maafisa wa Mahakama ya uhalifu wa kimataifa, ICC, amri ambayo ilipitishwa tarehe 11 Juni 2020 na aliyekuwa rais wa nchi hiyo wakati huo Donald Trump. Agizo la sasa la kufuta amri hiyo dhidi ya watu hao wakiwemo Mwendesha Mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda.

ICC ina jukumu muhimu katika kuendeleza uwajibikaji kwa uhalifu wa kimataifa.” Katibu Mkuu Guterres ameeleza kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani. 

Kupitia taarifa hiyo, Katibu Mkuu Guterres amethibitisha kuendelea kwa ushirikiano wa Umoja wa Mataifa chini ya Mkataba wa Uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. 

Mwaka jana 2020 mwanzoni mwa mwezi Septemba, tangazo lililotolewa na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo lilieleza  kuweka vikwazo dhidi ya Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda na Phakiso Mochokocho ambaye Mkuu wa kitengo cha ICC kinachohusika na masuala ya mamlaka ya kimaeneo ya mahakama hiyo likidai kuwa msingi wake ni kwamba ICC katika utendaji wake inazidi kulenga raia wa Marekani.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter