Michezo inaweza kutufanya kurejea katika maisha yetu baada ya COVID-19 

5 Aprili 2021

Kuelekea siku ya Kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani kesho Aprili 6,  ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku hiyo umeeleza kuwa Mchezo unaweza kusaidia kuchukua jukumu katika kujenga mnepo na katika kupona dhidi ya janga la COVID-19. 

Siku ya Kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani huadhimishwa kila tarehe 6 Aprili na inatoa fursa ya kutambua jukumu ambalo michezo na shughuli za mwili zinafanya katika jamii na katika maisha ya watu ulimwenguni kote. 

"Janga la COVID-19 limefanya iwe vigumu kukusanyika kama marafiki, timu na mashabiki kushindana, kucheza na kushangilia pamoja." Umesema ujumbe huo.   

Awali, Umoja wa Mataifa uliwaomba watu kati ya Jumatano, 31 Machi, hadi kesho Jumanne, Aprili 6, kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii kuweka picha au video inayoonesha thamani ya mchezo maishani na kuonesha umuhimu wa kuhakikisha kuwa sote tunalindwa na COVID- 19. Washirikia wameombwa kutumia kitambulisha mada yaani hashtags #OnlyTogether yaani ni Kwa pamoja tu tunaweza kucheza au kufurahi tena. 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter