Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaendeleza mshikamano kwa Timor-Leste iliyokumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa 

Picha ya kutoka angani karibu na mji mkuu wa Timor-Leste, Dili. (Maktaba)
UN Photo/Martine Perret
Picha ya kutoka angani karibu na mji mkuu wa Timor-Leste, Dili. (Maktaba)

UN yaendeleza mshikamano kwa Timor-Leste iliyokumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa 

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa nchini Timor-Leste na washirika wa misaada ya kibinadamu wamejitolea kuunga mkono hatua za kitaifa  katika kuratibu mwitikio wa dharura dhidi ya mafuriko mabaya zaidi yaliyoripotiwa hivi karibuni nchini humo. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanakabidhi vitu vya msaada kwa Kurugenzi ya Ulinzi wa Raia ya nchi hiyo ili viweze kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo.  

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa katika nchi hiyo ya Timor-Leste iliyoko kusini-mashariki mwa bara la Asia, inasema mojawapo ya mvua kubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni ya Timor-Leste imeathiri vibaya nchi nzima, pamoja na mji mkuu wa Dili, na kusababisha mafuriko mabaya zaidi na maporomoko ya ardhi vilivyodsababisha vifo kadhaa, kuziacha familia kadhaa bila makazi, na wengine  

Pia kuna ripoti za uharibifu mkubwa kwa nyumba na miundombinu muhimu, pamoja na barabara,  

"Umoja wa Mataifa huko Timor-Leste umesikitishwa sana na kupoteza maisha na miundombinu iliyosababishwa na janga la asili. Mafuriko haya pia yameathiri wafanyakazi wengi na familia za Umoja wa Mataifa. Kwa niaba ya timu ya Umoja wa Mataifa, natoa pole za dhati kwa wale walioathirika. Tunafuatilia hali hiyo kwa uangalifu sana. Timu ya Umoja wa Mataifa na washirika wa misaada ya kibinadamu wamejitolea kuunga mkono harakati za kitaifa kwa kuunga mkono hatua zote zinazoweza kutokea za dharura.” Amesisitiza Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Roy Trivedy. 

Mamlaka ya Ulinzi wa Kiraia imetoa taarifa zaidi kuwa vifo kadhaa pia wameripotiwa kutoka sehemu kadhaai za nchi. Wamesema, "ni vigumu wakati huu kutathmini idadi ya uharibifu kwani mvua inaendelea siku ya 4 mfululizo." Serikali pia ilikuwa na wasiwasi juu ya uharibifu uliosababishwa na miundombinu ya kuzuia na kushughulikia masula ya COVID-19, pamoja na Maabara ya Kitaifa na vituo viwili vya karantini huko Vera Cruz na Tasitolu ambayo ni maeneo ya mji mkuu, Dili.