Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa Benki ya Dunia Afghanistan wasaidia wanawake kuinua maisha yao 

Wanawake wa Afghanistan wakitembea Kishm kijijini Badakshan
UNAMA/Torpekai Amarkhel
Wanawake wa Afghanistan wakitembea Kishm kijijini Badakshan

Mradi wa Benki ya Dunia Afghanistan wasaidia wanawake kuinua maisha yao 

Ukuaji wa Kiuchumi

Nchini Afghanistan, mradi wa pamoja wa Benki ya Dunia na wakfu wa ujenzi mpya wa taifa hilo, ARTF umesaidia wanawake kuweza kudai haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi inayotambulika kisheria na sasa kuwawezesha wale wanaomiliki ardhi siyo tu kuwa na maisha bora zaidi bali pia thamani ya ardhi wanayomiliki kuongezeka kutokana na hatimiliki.

Nchini Afghanistan katika eneo la Qala-e-Fatou, Zia Jan, akimfundisha mwanae kusoma na kuandika. 

Zia anasema kwa muda mrefu amekumbwa na masahib kutokana na kutomiliki nyumba. “Mapema alfajiri kabla sijaenda kwenye mihangaiko yangu, lakini nifagie uwanja la sivyo baba mwenye nyumba anakasirika. Kitendo cha wakati mwingine kuchelewa kulipa kodi ya nyumba, ndio kinamfanya awe na hasira zaidi. Nilijenga nyumba hii kwa akiba ya ujira wangu. Nilinunua ardhi kwa dola 3,000 za kimarekani na kila mwaka nilikuwa najenga chumba kimoja.” 

Kwa wanawake nchini Afghanistan, sheria inawapatia haki sawa ya kumiliki ardhi na mali, lakini wengi wao kama ilivyokuwa kwa Zan wananyimwa haki hiyo kwa kushindwa kufuatilia, lakini sasa mradi wa Benki ya Dunia na ARTF umewafungua macho na wamedai nyaraka zao za umiliki. “Ilikuwa ni wakati wa majira ya baridi maafisa ARTF walifika kupima na kuchukua picha, wakanieleza kuwa nyaraka zangu zikiwa tayari nitapigiwa simu. Nilipigiwa simu nikaenda kuchukua nyaraka zangu kutoka wilayani. Ukiwa na nyaraka, mtu hawezi kudai kuwa mali hii ni yake. “ 

Sasa hata thamani ya ardhi ya Zia imeongezeka kutoka dola Elfu 7 hadi dola Elfu 12. 

Zia anasema mara nyingi wanawake wanaonekana hawana uwezo, lakini wanaweza kufanya kazi kuliko wanaume, na kwamba wanawake uwezo wao mara nyingi wanapuuzwa na juhudi zao hazionekani.