Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasyria 9 kati ya 10 wanaishi kwenye umaskini, tuwasaidie – Guterres

Familia iliyokimbia makazi yao, wakiwa katika hema la muda katika kambi kaskazini mwa vijijini Aleppo, Syria.
© UNICEF/Ali Almatar
Familia iliyokimbia makazi yao, wakiwa katika hema la muda katika kambi kaskazini mwa vijijini Aleppo, Syria.

Wasyria 9 kati ya 10 wanaishi kwenye umaskini, tuwasaidie – Guterres

Msaada wa Kibinadamu

Kupitia katika ujumbe wa video kwa Mkutano wa tano unaofanyika Brussels, Ubelgiji,  kuunga mkono Syria na ukanda huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa wafadhili kusaidia kushughulikia mahitaji yanayoongezeka na kuongeza ahadi za kifedha na kibinadamu kuwasaidia Wasyria na "kupunguza mzigo mkubwa wa kifedha wa nchi ambazo zinahifadhi wakimbizi.” 

Guterres alimesema, "kwa miaka kumi, Wasyria wamevumilia kifo, uharibifu, kufurushwa na kupunjwa. Mamia ya maelfu ya raia wameuawa na mamilioni wamejeruhiwa. Zaidi ya nusu ya idadi ya watu wamelazimishwa kutoka katika nyumba zao. Wengine wengi wamekufa kwa njaa chini ya kuzingirwa, kuteswa, kuzuiliwa kinyume cha sheria, au kutoweshwa kwa nguvu.” 

Guterres ameendelea kueleza kuwa nusu ya watoto nchini Syria wamezaliwa vitani na hawajui chochote kingine, “zaidi ya watoto milioni 2 wa Syria ni wakimbizi. Wanabeba vidonda vya kisaikolojia ambavyo vitaendelea maisha yote. Na mambo yanazidi kuwa mabaya, sio bora. Zaidi ya watu milioni 13 wanahitaji msaada wa kibinadamu kuishi mwaka huu. Hiyo ni zaidi ya asilimia 20 zaidi ya mwaka jana na idadi kubwa ya watu sasa wanakabiliwa na njaa. Watu wengine milioni 10.5 wakimbizi wa Syria na wale wanaowakaribisha wanahitaji msaada katika eneo lote. Uchumi wa Syria umeharibiwa na sasa athari za COVID-19 zimefanya mambo kuwa mabaya zaidi. Karibu nusu ya familia zote zilipoteza chanzo cha mapato. Wasyria tisa kati ya kumi wanaishi katika umaskini.” 

Mkutano wa Brussels, ulioandaliwa na Jumuiya ya Ulaya, unatafuta ahadi hadi $ 10 bilioni kutoka kwa wafadhili, $ 4.2 bilioni kwa watu nchini Syria na $ 5.8 bilioni kwa wakimbizi na wenyeji wao. 

Aidha Katibu Mkuu Gutrerres amesema, "kwa wengi, misaada ya kibinadamu na ulinzi ulioletwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wetu wa kibinadamu ndio chanzo chao pekee cha kuishi. Kila mwezi, watoa misaada ya kibinadamu huleta msaada kwa watu milioni 7.6 nchini Syria. Hii ni shukrani inayowezekana kwa kujitolea na uvumilivu wa ajabu wa wanadamu na wafanyakazi wa afya katika mstari wa mbele. Wengi wao ni Wasyria ambao wao wenyewe wameteseka kwa sababu ya mzozo. Wana ujasiri mkubwa sana, na maelfu yao wameuawa, wamelemazwa, wanazuiliwa na kutekwa nyara tangu mzozo ulipoanza. Baada ya miaka kumi ya vita, Wasyria wengi wamepoteza imani kwamba jamii ya kimataifa inaweza kuwasaidia kuunda njia iliyokubaliwa kutoka kwa mzozo. Nina hakika kwamba bado tunaweza, pamoja na vyama vya Syria wenyewe." 

Katika mkutano wa mwaka jana huko Brussels, wafadhili waliahidi ufadhili wa dola bilioni 5.5 kusaidia shughuli za kibinadamu, uthabiti na maendeleo katika mwaka 2020.