Asilani hakuna mwanangu atakaye keketwa! 

29 Machi 2021

Kama asilimia 95 ya wanawake wanawake katika jamii yake chini Uganda, wamekeketwa. Margaret Chepoteltel alikeketwa  (FGM) utotoni na kutumbukia katika madhara ya kiafya katika maisha yake yote.  

Kwa sasa chini ya mradi unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa, anahamasisha jamii yake kuhusu madhara ya ukeketaji kwa wanawake. 

‘Sijawahi kuhisi maumivu makali ya kupindukia maishani mwangu’ 

“Leo, nakemea ukeketaji wa wanawake, lakini nilipokuwa mtoto niliitamani. Nilikuwa nafikiri kwamba inamaanisha kuwa tayari kwa ajili ya kuolewa na kuweza kutimiza mapenzi ya wazazi wangu kwa sababu mwanamke aliyekeketwa huolewa kwa kulipiwa mahari kubwa zaidi kuliko yule asiyekeketwa. Nilifanyiwa nilikeketwa au kufanyiwa (FGM) nikiwa na umri wa miaka 13 na miaka miwili badaaye, niliozeshwa na nikaenda kuishi katika familia ya mme wangu.” 

Baada ya miaka miwili katika ndoa, nilipata ujauzito uliofuatiwa na matatizo mengi wakati wa kujifungua.  

Nililazimika kutembea safari ndefu hadi kwenye kituo cha afya kilichonidhoofisha sana. 

Nilishindwa kusukuma mtoto , kwani hakuweza kupita hali iliypolazimisha mkunga kuniongeza njia ili mtoto apite na nikavujwa  na damu nyingi sana.  

Sijawahi kuhisi maumivu makalli zaidi katika maisha yangu yote. Nilinusurika kifo lakini nilimpoteza mwanangu mchanga . 

Sikujua kwamba matatizo wakati wa kujifungua na mengine ya kiafya yalikuwa na uhusiano na ukeketaji wa wanawake.  

Mwishowe nilibaini hilo nilipowasiliana na mfuko wa shirika la Mawasiliano wa ajili ya maendeleo nchini yani Communication for Development Foundation Uganda (CDFU), na pia baada ya kuhudhuria mkutano kuhusu athari za ukeketaji wa wanawake (FGM). 

Margaret Chepoteltel ambaye alikeketwa akiwa msichana mdogo.
CDFU/John Bosco Mukura
Margaret Chepoteltel ambaye alikeketwa akiwa msichana mdogo.

Kutokomeza FGM kabisa 

Kwa sasa mimi ni mama wa watoto wawili wa kike, mmoja akiwa na umri wa miaka saba na mwingine miaka nane.  

Kila ninapowaona nafikiria wao kupitia kile nilichopitia na moyo wangu huvunjika na kuishiwa nguvu.  

Hua ninawambia kuhusu hatari ya kukeketwa, na pia nimeapa kwamba asilani sitaki kuona binti yangu yoyote anapitia mchakato huu uliotia doa maishja yangu yote.  

Mwanamume akishika bango lenye tamko la kuachana na ukeketaji kwenye kijiji cha Naturongole nchini Uganda.
UNICEF/Henry Bongyereirwe
Mwanamume akishika bango lenye tamko la kuachana na ukeketaji kwenye kijiji cha Naturongole nchini Uganda.

Baadaye nilipokea mafunzo ya kijamii na sasa ninapigania utokomezwaji kabisa wa FGM katika kijiji changu  cha Luchengenge, katika wilaya ya Amudat mashariki mwa Uganda.  

Nilikuwa nikiogopa muitikio wa jamii ninapotaka kuongea kuhusu suala hili lakini sasa najihisi nimewezeshwa kusema maneno ya kupinga na kutokomeza kabisa FGM. 

Ikizingatiwa kwamba kwa sasa nina jukwaa, nitaendelea kuhamasisha na kutoa ushuhuda dhidi ya tohara ya wanawake, hata kwa wanaume, kwa sababu ninajua madhara yake.  

Nikinyamaza inamaanisha binti zetu wataendelea kupitia machungu makubwa na utesaji.  

“Ni lazima tuendelee kuwaambia kinamama na baba wazazi na wasichana wenyewe kuhusu madhara ya FGM, na kupinga ukeketaji. Sitaacha kampeni ya kuoa maisha”. 

Margaret Chepoteltel alikuwa akiongea kwneye Spotlight Initiative  ambao ni mradi wa a shirka la Umoja wa Mataifa na Muungano wa Ulaya (EU) kutokomeza aina zote za ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. 

 

Ngariba nchini Uganda ambaye sasa anaunga mkono juhudi za kutokomeza ukeketaji.
UNICEF/Nakibuuka
Ngariba nchini Uganda ambaye sasa anaunga mkono juhudi za kutokomeza ukeketaji.

 

Umoja wa Mataifa na vita dhidi ya FGM 

  • Umoja wa Mataifa na vita dhidi ya FGM  

Umoja wa Mataifa unasema, kwamba COVID-19 imeathiri vibaya wasichana na wanawake, na kusababisha kile kiitwacho “mlipuko wa kivuli” uliokwamisha utokomezaji wa mila potofu zote ikiwemo FGM.  

  • Katika mwaka 2018, ilikadiriwa na shirika la idadi ya watu la  Umoja wa Mataifa (UNFPA) kwamba wasichana milioni 68 walikuwa hatarini; na sasa makadirio haya yamesimama kwa milioni 70.  
  • Kazi ya Chepoteltel katika kijiji chake ni sehemu ya mradi wa Communication for Development Foundation Uganda (CDFU) wa “Furahisha Usitende Ukatili”, kampeni inyoungwa mkono na Spotlight Initiative na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women.  
  • UN Women inaisaidia CDFU kama msihirki wa utekelezaji kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana nchini Uganda.  
  • Kampeni zinazoungwa mkono zinatekelezwa kupitia vyombo vya habari na na uhamasishaji wa kijamii, zikiwalenga watu binafsi, jamii na tasisi ili washiriki katika kampeni za kukuza mila chanya, mtazamo na kupinga mila potofu. 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter