Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa UN lazima walindwe wanapofanya kazi ya kuokoa maisha:Guterres

Bendera ya Un ikipoepea nusu mlingoti kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini New York Marekani kuwakumbuka wafanyakazi waliopoteza maisha yao kwenye machafuko Gaza
UN Photo/Mark Garten)
Bendera ya Un ikipoepea nusu mlingoti kwenye makao makuu ya shirika hilo mjini New York Marekani kuwakumbuka wafanyakazi waliopoteza maisha yao kwenye machafuko Gaza

Wafanyakazi wa UN lazima walindwe wanapofanya kazi ya kuokoa maisha:Guterres

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi zote kuunga mkono mkataba wa kimataifa wa kuwalinda wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa  na wanaohusiana na Umoja huo ili kuhakikisha wale wote wanaofanya kazi muhimu za shirika hilo wana usalama wanaouhitaji kutimiza majukumu yao.

Antonio Guterres ametoa ujumbe huo katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya mshikamano na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaoshikiliwa au walio toweka,huku akielezea hatari kubwa inayowakabili wahudumu na wafayakazi wa Umoja wa Mataifa kote duniani.

"Vitisho vinatofautiana kuanzia kwa kuwavizia kwa makusudi na kuwaua hadi utekaji nyara, kuwatisha na kuwekwa kizuizini kinyume cha sheria. Lakini uzi ni ule ule, hivi ni vikwazo visivyokubalika kutimiza majukumu yetu na kuendeleza amani, maendeleo endelevu, haki za binadamu na misaada ya kibinadamu kote ulimwenguni. Wafanyikazi wa kitaifa mara nyingi ndio walio katika hatari fulani ”, ameongeza kusema Katibu Mkuu.

Wafanyikazi 20 wa UN waako kizuizini

Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa “hadi kufikia tarehe 15 Machi, wafanyikazi 20 wa Umoja wa Mataifa wako kizuizini, pamoja na sita ambao walikamatwa mwaka huu, watano mwaka 2020, na wengine kabla ya hapo.”

Operesheni za kulinda amani ndio mlengwa mkubwa haswa, ambapo wafanyikazi wasiopungua 10 wamepoteza maisha mwaka huu kwa mashambulizi mabaya kabisa.

Siku ya Kimataifa inafanyika wakati wa kumbukumbu ya kutekwa nyara kwa Alec Collett, ambaye alichukuliwa na watu wenye silaha mnamo mwaka 1985 wakati akifanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa Wakimbizi wa Palestina huko Mashariki ya Karibu (UNRWA). 

Mwili wake hatimaye ulipatikana katika Bonde la Bekaa nchini Lebanoni mwaka 2009.

Siku hii pia inaenzi kumbukumbu yake, na ile ya wale wote ambao wamepitia hali kama hiyo.

Lazima tufanye kila tuwezalo’

Katika ujumbe wake, Bwana Guterres amezitaka nchi zote kuunga mkono Mkataba wa 1994 wa kuhusu Usalama wa Umoja wa Mataifa na wafanyikazi wanaohusika na vile vile itifaki yake ya hiari ya mwaka 2005, ambayo inatoa ulinzi kwa wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa wanaotoa misaada ya kibinadamu, kisiasa au maendeleo.

Hadi sasa, ni nchi 95 tundizo shememu ya mwanachama wa mkataba huo, na ni nchi 33 zilizoridhia itifaki yake..

Amesisitiza kwamba Shirika la Umoja wa Mataifa "litaendelea na juhudi zake za kulinda wafanyikazi wetu, na kufuata haki kwa wahusika wa mashambulizi" na ameishukuru kamati ya kudumu ya usalama na uhuru wa huduma ya kiraia ya kimataifa ya jumuia ya wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa kwa utetezi wake na umakini.”

Kwa mantiki hiyo amekumbusha “Kwa pamoja ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba wale ambao wanafanyakazi za kuokoa maisha kote duniani wana ulinzi na mazingira wanayohitaji kuweza kutimiza majukumu yao muhimu.”