Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka kwa wiki ya nne mfululizo ingawa vifo vimepungua:WHO

Peru imepokea dozi 117,000 za chanjo dhidi ya COVID-19 kupitia mkakati wa chanjo wa COVAX kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chaves
© UNICEF/Jose Vilca
Peru imepokea dozi 117,000 za chanjo dhidi ya COVID-19 kupitia mkakati wa chanjo wa COVAX kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chaves

Maambukizi ya COVID-19 yaongezeka kwa wiki ya nne mfululizo ingawa vifo vimepungua:WHO

Afya

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 imeendelea kuongezeka kote dunini kwa wiki ya nne mfululizo huku wagonjwa milioni 3.3 wapya wakiripotiwa katika siku saba zilizopita limesema leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.

Shirika hilo limeongeza kuwa idadi ya vifo vipya kutokana na virusi vya corona imesalia kutoongezeka sana baada ya kupungua kwa wiki sita mfululizo ambapo vifo vipya ni 60,000 viliripotiwa.
Ulaya na Amerika ziliendelea kuongoza kwa karibu wagonjwa wanane kati ya 10 wapya na vifo vyote, wakati eneo pekee lililoripoti kupungua kwa vifo ni Pasifiki Magharibi, ambako vifo vimepungua chini ya theluthi moja, ikilinganishwa na wiki zilizopita.

Hakuna ukanda uliosalimika

Kwa mujibu wa WHO maambukizi yameongezeka haswa katika Asia ya Kusini Mashariki, Pasifiki ya Magharibi, Ulaya na Mediterania ya Mashariki, kulingana na taarifa za kila wiki za mwenendo wa maambukizi wa shirika hilo.
Katika ukanda wa Afrika na Amerika, idadi ya maambukizo imebaki imara katika wiki za hivi karibuni ingawa WHO imeonyesha hofu "kuhusu mwenendo" katika baadhi ya nchi zingine ndani ya maeneo haya.
Nchi hizo ni pamoja na Brazil, ambapo idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wapya mpya imeripotiwa (wagonjwa wapya 508,010 kwa wiki, likiwa ni ongezeko la asilimia tatu)
Msrekani imeshuhudia wagonjwa wapya 374,369 likiwa ni punguzo la asilimia 19, wakati India imepata wagonjwa wapya 240,082, ambalo ni ongezeko la asilimia 62, Ufaransa imepata visa vipya 204,840 (ongezeko la asilimia 27) na Italia imeona mabadiliko kidogo, kwa wagonjwa wapya 154,493 walioripotiwa .

Mama na mwanae aliyezaliwa wakati wa COVID-19 Gujarat, India.
© UNICEF/Vinay Panjwani
Mama na mwanae aliyezaliwa wakati wa COVID-19 Gujarat, India.

Wasiwasi kuhusu aina tofauti za virusi

WHO imesema kwamba takwimu mpya za kuhusu aina tofauti ya virusi vinavyotia hofu zinaonyesha kwamba aina inayoitwa ya "Uingereza" iko katika nchi 125, katika mabara yote sita ya ulimwengu.
Aina hii VOC202012 / 01  inaweza kuhusishwa na hatari kubwa ya kulazwa hospitalini, kuugua mahtuti na vifo, imesema WHO, ikionyesha utafiti unaohusisha wagonjwa 55,000 wa COVID-19 kati ya Oktoba mwaka jana na Januari mwaka huu, ambapo vifo kutokana na aina hiyo ya Uingereza vilikuwa ni watu 4.1 kwa kila watu 1,000 , ikilinganishwa na watu 2.5 kwa kila watu 1,000 kati ya wale walioambukizwa virusi vya corona viliyosambaa hapo awali.

Ufanisi wa chanjo

Kwa upande wa maoni mazuri zaidi, takwimu za majaribio ya chanjo iliyofanyika England kuanzia Desemba 2020 hadi Februari 2021 wakati anina ya VOC202012 / 01 ya virusi ilikuwa imeenea sana  "ilionyesha ufanisi wa mapema duniani kote wa chanjo aina ya Pfizer / BioNTech - BNT162b2 na chanjo ya AstraZeneca - ChAdOx1 dhidi ya waghonjwa wa COVID-19, waliothibitishwa,  kulazwa hospitalini na vifo ”, limeeleza shirika la WHO 

Muuguzi akiwasalimu wageni katika kliniki iliyowekwa kwenye hospitali nchini Thailand kwa ajili ya wagonjwa wenye dalili za COVID-19
WHO/P. Phutpheng
Muuguzi akiwasalimu wageni katika kliniki iliyowekwa kwenye hospitali nchini Thailand kwa ajili ya wagonjwa wenye dalili za COVID-19


Aina ya virusi ya 501Y.V2 inajulikana sana

Aina inayoitwa "Afrika Kusini" - 501Y.V2  sasa iko katika nchi 75 katika mabara yote.
Ikiangazia matokeo ya utafiti kwa kulinganisha wagonjwa waliolazwa hospitali nchini Afrika Kusini wakati wa kilele cha wimbi la kwanza la maambukizi ya virusi vya corona katikati ya Julai 2020 na wimbi la pili ambalo lilifika Januari 2021 wakati aina tofauti ya 501Y. V2 iliposambaa zaidi WHO imeonyesha kwamba "hatari ya vifo vya hospitalini iliongezeka kwa