Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yaadhimisha Siku ya ushairi duniani kwa kuonesha nguvu ya ubunifu. 

sanaa
UNESCO
sanaa

UNESCO yaadhimisha Siku ya ushairi duniani kwa kuonesha nguvu ya ubunifu. 

Utamaduni na Elimu

Siku ya Ushairi Duniani, inayoadhimishwa kila tarehe 21 ya mwezi Machi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linakumbusha kwamba ushairi unaheshimika katika tamaduni zote kupitia historia na kwamba ni moja wapo ya aina tajiri zaidi ya utamaduni, kujieleza kwa lugha na utambulisho.

Maadhimisho haya yanalenga kuhamasisha usomaji, uandishi na ufundishaji wa mashairi kwa kukuza mazungumzo ya kitamaduni na densi, sanaa ya maigizo na uchoraji. 

Moja ya malengo makuu ya Siku hii ni kusaidia utofauti wa lugha kupitia ughani wa mashairi na kuzipatia lugha zilizo hatarini, uwezekano wa kusikika katika jamii zao. 

Kwa mujibu wa UNESCO, ushairi ni mshirika mkuu wa uelewa kati ya watu. Kichocheo cha amani na mazungumzo. 

Katika hafla hii, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay, amesema kuwa mashairi yana uwezo wa kukumbusha kila mtu juu ya mnepo wa roho ya mwanadamu. 

Mwaka mmoja uliopita, mwanzoni mwa janga hilo, UN News iliwataka washairi, waandishi na wapenzi wa mashairi ulimwenguni kote kusimulia katika aya jinsi shida ya COVID-19 imewaathiri. 

Siku ya Ushairi Duniani iliundwa mnamo 1999 wakati wa kikao cha 30 cha UNESCO huko Paris, Ufaransa.