Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

 Hongera Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na waandishi wa habari, New York.
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na waandishi wa habari, New York.

 Hongera Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania:Guterres

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amempongeza muheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa kama Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Antonio ametoa pongezi hizo kupitia taarifa iliyotolewa mchana wa leo na msemaji wake mjini New York Marekani.

Katika taarifa hiyo Kastibu Mkuu amesema anatarajia kufanyakazi kwa karibu na Rais huyo ikiwemo kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDG.

Bi. Sukuhu Hassan ameapishwa kushika mamlaka hayo baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Joseph Pombe Magufuli kufariki dunia Machi 17 kutokana na matatizo ya moyo.

Familia ya UN inakupongeza

Naye mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milišić, amempongeza rais wa sita wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuapishwa leo rasmi na kuwa rais wa kwanza mwanamke katika taifa hilo. 

Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter mwakilishi mkazi huyo amesema Umoja wa Mataifa nchini Tanzania uko tayari kufanya kazi na serikali yake na kumtakia kila la heri.