Vikosi vya usalama nchini Myanmar vyakalia maeneo ya shule, UN yalaani.

19 Machi 2021

Vikosi vya usalama nchini Myanmar vimeripotiwa kukalia zaidi ya shule 60 na maeneo ya vvyuo vikuu kote nchini humo, kuashiria kuongezeka kwa mgogoro huo, Shirika la Umoja wa Mataiafa la kuhudumia Watoto UNICEF, limesema leo IIjumaa.

Katika taarifa iliyotolewa baadaye, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani "vurugu za kikatili" zilizoelekezwa kwa waandamanaji wa amani wakati idadi ya vifo ikioongezeka.

"Mauaji ya waandamanaji wa amani na ukamataji holela, ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari, hayakubaliki kabisa.” Amesema António Guterres katika taarifa iliyotolewa na Msemaji wake mjini New York Marekani.

Bwana Guterres ameongeza kusema, "'mwitikio imara wa pamoja, unahitajika kwa haraka, jeshi linaendelea kukataa wito, ikiwa ni pamoja na wito wa Baraza la Usalama, ili kukomesha ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu na kurudi katika njia ya demokrasia. Hatua ya kimataifa ya haraka inahitajika.”

Shirika la elimu, sayansi naa utamaduni UNESCO, limesema katika tukio moja, vikosi vya usalama viliripotiwa kuwapiga walimu wawili wakati wakiingia kwenye majengo ya shule, na kuwajeruhi wengine.

UNESCO, UNICEF na Save the Children wameonya kuwa  hali hiyo itaongeza mgogoro wa kujifunza kwa karibu watoto milioni 12 na vijana nchini Myanmar, ambao tayari ulikuwa chini ya shinikizo kubwa kutokana na janga la COVID-19.

Ondokeni kwenye majengo haraka

Aidha mashirika hayo yametoa wito kwa vikosi vya usalama kuondoka haraka katika majengo ya shule na

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter