Mabilioni ya watu kuishi bila maji na usafi ni ni kuporomoka kwa maadili:UN

Mama akiwa amebema mwanaye mgogoni akichota maji karibu na hospitali ya Sipera Bulawayo Zimbabwe 6 Juni 2018
UNDP/Karin Schermbrucker for Slingshot
Mama akiwa amebema mwanaye mgogoni akichota maji karibu na hospitali ya Sipera Bulawayo Zimbabwe 6 Juni 2018

Mabilioni ya watu kuishi bila maji na usafi ni ni kuporomoka kwa maadili:UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Upatikanaji wa maji sio tu suala la kuwa na kimiminika kwenye chupa lakini badala yake linagusa maswala ya ulimwengu kama vile utu, fursa na usawa, amesema Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu kuhakikisha maji na usafi wa mazingira vinapatikana kwa watu wote.

Kwa Volkan Bozkir, majadiliano yalikuwa yamepitwa na wakati, ikizingatiwa takwimu kama vile watu bilioni tatu ulimwenguni bado hawana vifaa vya msingi vya kunawa mikono, hata katikati ya janga hili la COVID-19.
"Endapo ntaweza kusema ukweli hilo ni kutofaulu kwa maadili tunayoishi katika ulimwengu huu wenye viwango vya juu vya ubunifu na mafanikio, lakini tunaendelea kuruhusu mabilioni ya watu kuishi bila maji safi ya kunywa au zana za msingi za kunawa mikono ," asema Rais huyo wa Baraza Kuu.

Hakuna kisingizio cha kuchukua hatua

Mkutano huo umeujikita katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo yanayohusiana na maji ya katika ajenda ya 2030, mwongozo wa ulimwengu bora, na endelevu zaidi. 
Moja ni kuhakikisha na kuahidi kutomwacha mtu yeyote nyuma, na Lengo la maendeleo endelevu namba 6  (SDG6) ambalo linazungumzia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira.

Kisima cha kwanza kabisa cha maji kujengwa katika kijiji cha Chikwala wilaya ya Mazabuka jimboni Luapula nchini Zambia. Ni chanzo cha maji safi na salama kwa kaya 600.
© UNICEF/UN0391492/Siakachoma/OutSet Media
Kisima cha kwanza kabisa cha maji kujengwa katika kijiji cha Chikwala wilaya ya Mazabuka jimboni Luapula nchini Zambia. Ni chanzo cha maji safi na salama kwa kaya 600.

Kwa kuongezea, mkutano huo wa Baraza Kuu umetangaza miaka kumi yaani kuanzia 2018 hadi 2028, kuwa ni muongo wa kuchukua hatua kwa ajili ya maji, ambao pia unashughulikia kuongezeka kwa shinikizo la kimataifa kuhusu rasilimali za maji, na kuzidisha hatari ya ukame na mafuriko.
Bwana Bozkir amesema ukweli kwamba wakati wa janga la COVID-19, mabilioni hawajapata vifaa vya msingi vya kunawa mikono, wakati wafanyikazi wa afya katika baadhi ya nchi zilizo na maendeleo duni kabisa hawana maji ya bomba, inawakilisha "mfano dhahiri wa ukosefu wa usawa duniani ambao unahitaji hatua.”
"Ingawa hatuwezi kurudi nyuma na kubadilisha kile kilichotokea, lazima tutambue makosa yetu na tutumie fursa hii kuondoa mapengo ya kimfumo ambayo yameruhusu changamoto hii kushamiri", amesema bwana Bozkir.
Ameongeza kuwa "Wakati janga au mgogoro mwingine utakapotokea duniani, na tunajua kwamba itakuwa hivyo, hatutakuwa na kisingizio cha  kutochukua hatua sasa."
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa upande wake amesisitiza jinsi ulimwengu ulivyo mbali katika kufikia leongo la SDG 6. 
Amina Mohammed ameuambia mkutano huo kiwango cha sasa cha maendeleo kinapaswa kuongezeka mara nne ili kuweza kuyafikia malengo hayo katika tarehe ya ukomo ya 2030.

Wasichana wakibeba maji Yangambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.
CIFOR/Axel Fassio
Wasichana wakibeba maji Yangambi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

Shughulikia pengo la usawa

"Kwa kuongezea, changanoto za dunia, pamoja na vitisho vilivyohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa bioanuwai na uchafuzi wa mazingira, zitaongeza uhaba wa maji. Kufikia mwaka 2040, mmoja kati ya watoto wanne duniani walio chini ya miaka 18 sawa na watoto milioni 600 watakuwa wakiishi katika maeneo yenye matatizo ya uhaba wa maji." Amesema naibu Katibu Mkuu.
Bi Mohammed ameangazia pia masharti matatu akizitaka nchi kutumia mipango yao ya kujikwamua na janga la COVID-19 kuwekeza katika SDGs na kushughulikia upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwa usawa.
Ameziomba pia serikali "kuongeza hasama yah atua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ", ikizingatiwa kuwa asilimia 90 ya majanga ya asili yanahusiana na maji, kama mafuriko, ambayo yanaweza kuchafua vyanzo vya maji.
Wanawake na wasichana wanaathirika zaidi
Hoja yake ya mwisho Bi. Mohammed ni wito wa usawa wa kijinsia, ikiwemo katika kufanya maamuzi.
Amesema "Wanawake na wasichana wanateseka sana wakati maji na usafi wa mazingira unapokosekana, yakiathiri afya na mara nyingi huzuia fursa za kazi na elimu. “
Lakini wanawake pia ni uti wa mgongo wa kilimo na wasimamizi wakuu wa maliasili amesema Bi Mohammed.
"Hatua za kupambana na janga la COVID-19 limeonyesha uwezo wa uongozi wa wanawake. Hebu tutumie uzoefu huu wakati sera zinawekwa ili kujenga uchumi unaojali mazingira.”