Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yalaani vikali mauaji ya kikatili ya raia 58 Niger

Mariama (kushoto) mwenye umri wa miaka 17 na Zeinabou mwenye umri wa miaka18 kutoka Niger wanasema walichukua hatua kuepusha ndoa ya mapema ya rafiki yao mwenye umri wa miaka 16.
© UNICEF/Juan Haro
Mariama (kushoto) mwenye umri wa miaka 17 na Zeinabou mwenye umri wa miaka18 kutoka Niger wanasema walichukua hatua kuepusha ndoa ya mapema ya rafiki yao mwenye umri wa miaka 16.

UNICEF yalaani vikali mauaji ya kikatili ya raia 58 Niger

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Msataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo limelaani vikali mashambulizi yaliyokatili makumi ya raia kwenye vijiji viwili Magharibi mwa Niger.

Kupitia taarifa ya mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Marie-Pierre Poirier “Kundi lisilojulikana la watu wenye silaha  limewaua takriban watu 58 katika vijiji vya Darey-dey na Sinegogar vilivyopo katyika jimbo la Tillabery.”

Waathirika wa shambulio

Ameongheza kuwa miongoni mwa waliopoteza maisha ni Watoto 6 wa umri wa kati ya miaka 11 na 17. “ Tumeshitushwa sana na kukasirishwa kwamba raia wakiwemo watoto ni miongoni mwa watu waliouawa.” Amesema Bi. Poirie.

Duru za Habari zinasema shambulio hilo lilifanyika Jumatatu wakati wanaume wenye silaha walipovamia magari manne yaliyiokuwa yakisafirisha wana vijiji kutoka kwenye gulio la kila wiki. 

Bi. Poirie amekumbusha kwamba mapema mwezi Januari mwaka huu katika jimbo hilohilo makundi yenye silaha yalifanya mashambulizi ya kuratibiwa katika vijiji vya Tchamo-Bangou na Zaroumdareye na kuua watu angalau 100 wakiwemo watoto 17 wa umri wa chinin ya miaka 16.

UNICEF imesema ongezeko la machafuko katika ukanda wa Sahel ya Kati limesababisha athari nyingi na kubwa kwa uhali wa Watoto, elimu yao, ulinzi na maendeleo.

Mama akiwa na watoto wake katika eneo la Monguno, Jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria (Picha ya maktaba)
OCHA
Mama akiwa na watoto wake katika eneo la Monguno, Jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria (Picha ya maktaba)

Ukosefu wa usalama umetapakaa

Eneo la Tillabery nchini Niger, liko karibu na mipaka ya nchi ya Mali na Burkina Faso, ambapo zaidi ya watu 95,000 wamelazimika kuhama makazi yao. 

Bi. Poirier amesema kuongezeka kwa ukosefu wa usalama kumezidisha mahitaji ya kibinadamu na kuzuia kuwafikia maelfu ya watu walioathirika.

"Kufikia wale wanaohitaji msaada inazidi kuwa changamoto. Vurugu zinaathiri maisha na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii ikiwemo elimu na huduma za afya. Ukosefu wa usalama unazidisha kuwaweka watu hatarini. Na wanawake na watoto wamebeba mzigo mkubwa wa vurugu hizo.”

Kwa jumla, watu milioni 3.8 nchini Niger, pamoja na watoto milioni mbili, wanahitaji msaada wa kibinadamu. 

Hali hiyo inazidishwa zaidi na athari za janga la COVID-19.

Bi Poirier amesema UNICEF inaendelea kushirikiana na Serikali na washirika wake kuwapa watoto na familia ulinzi muhimu, huduma za afya na huduma za elimu. 

Walakini, amesisitiza kuwa msaada na ushiriki wa kimataifa unahitajika haraka kukomesha vurugu ili wahudumu wa misaada ya kibinadamu waweze kuwafikia wale wanaohitaji.