Tunahitaji fursa ya kuwafikia haraka wahamiaji walioathirika na moto Yemen:IOM

Tunahitaji fursa ya kuwafikia haraka wahamiaji walioathirika na moto Yemen:IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limetoa wito wa kupewa fursa ya haraka ya kibinadamu kwenye kituo cha mahabusu cha wahamiaji kwenye mji mkuu wa Yemen, Sana'a ambako moto mkubwa umeripotiwa kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu mkubwa mwishoni mwa wiki.
IOM pia imetoa wito wa kuachiuliwa kwa wahamiaji wote wanaoshikiliwa katika kituo hicho kinachosimwamiwa na mamlaka ya masuala ya uhamiaji na uraia, [pamoja na ahadi ya kuhakikisha kuwa njia zingine salama za kuwahamisha wahamiaji hao.
Makumi ya wahamiaji hao wamearifiwa kujeruhiwa kujeruhiwa, na IOM katika ukurasa wake wa Twitter imeandika kuwa kuwa zaidi ya wahamiaji 170 wametibiwa majeraha "na wengi wamebaki katika hali mbaya."
Carmela Godeau, mkurugenzi wa kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa IOM amesema "athari yake ni ya kutisha".
Idadi kamili ya vifo au majeraha bado haijabainika.
Ikitambua kuwa karibu wahamiaji 900 walikuwa katika kituo hicho kilichokuwa na msongamano mkubwa wa watu wakati moto huo ukizuka , IOM imesema ilikuwa na wafanyikazi wake katika eneo hilo wakati moto huo ulipotokea karibu na jengo kuu, kwenye kona ambapo kulikuwa na watu zaidi ya 350.

Pamoja na wizara ya afya ya Umma, timu za wafanyikazi wa afya wa IOM na magari ya kubeba wagonjwa, pamoja na vifaa 23,000 vya matibabu vilitumwa mara moja kwenye kituo hicho na katika hospitali ili kutoa msaada wa kuokoa maisha.
Afisa huyo wa IOM ametoa pole kwa familia za wale waliokufa, na ameomba kwamba jamii ya wahamiaji huko Sana'a wapewe nafasi ya "kuomboleza na kuzika wapendwa wao kwa heshima", na kuongeza kuwa UN iko tayari kutoa nyongeza ya msaada.
"Tunakabiliwa na changamoto za kuwafikia waliojeruhiwa kwa sababu ya kuongezeka kwa usalama katika hospitali", ameonya Bi Godeau, akisisitiza kwamba watoa misaada na wahudumu wa afya lazima wapewe fursa ya kuwatibu walioathiriwa na moto na wengine ambao wamekuwa wakipokea huduma kwa muda mrefu.
Ameongeza kuwa "Kwa kuwa wahamiaji wengi wako katika hali mbaya, kukidhi mahitaji yao ya kiafya lazima iwe kipaumbele cha haraka".
Yemen inatumika kama kituo cha kusafiri kwa maerlfu kwa maelfu ya wahamiaji wanaosafiri kati ya Pembe ya Afrika na Saudi Arabia.
Hata hivyo vikwazo vya usafiri vilivyotokana na janga la COVID-19 vimepunguza kiasi idadi ya wahamiaji wanaosafiri kutoka Zaidi ya 138,000 mwaka 2019 hadi zaidi kidogo ya 37,500 mwaka 2020.