Wahamiaji lazima wajumuishwe katika mipango ya chanjo ya COVID-19

8 Machi 2021

Wataalam wa masuala ya haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa, Afrika, Ulaya na muungano wa mfumo wa haki za binadamu Marekani wametoa mwongozo mpya ukitaka lazima wahamiaji wote wajumuishwe katika programu za jancho dhidi ya corona au COVID-19.

Katika mwongozo huo uliotolewa leo mjini Geneva Uswis, wataalam hao wamesisitiza kwamba “uandikishaji wa kupata chanjo usitumike kukusanya taarifa kuhusu hali ya uhamiaji ya wat una kusiwasilisha taarifa hizo kwa mamlaka zinazohusika na masuala ya uhamiaji.”

Mwongozo huo ulioandaliwa kwa pamoja na kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu wafanyakazi wahamiaji (CMW), mtaalam maaulm wa haki za binadamu za wahamiaji, ofisi ya kamishina mkuu wa haki za binadamu OHCHR na wataalam wa kikanda wa haki za binadamu unatoa mapendekezo 6 kuhusu usambazaji wa chanjo.

Unatoa wito kwa mataifa kuzingatia udhaifu, hatari na mahitaji ya wahamiaji hao ambao wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona au COVID-19  wakati wa kuandaa mikakati ya vipaumbele vyao vya chanjo.

© UNICEF/Juan Haro
Wanawake wahamiaji na wanao kwenye kituo cha karantini Niamey, Niger.

 “Katika muktadha wa janga la COVID-19, haki za afya na kutobaguliwa ni za msingi na za lazima. Ili kushinda janga hili na kutomuacha mtu yeyote nyuma, haki hizi lazima zihakikishwe kwa wahamiaji wote bila kujali utaifa na hali yao ya uhamiaji. Wahamiaji wote lazima wapate chanjo hiyo kwa usawa kama walivyo rai awa kawaida, ”wamesisitiza wataalam hao.

Wameongeza kuwa "Ripoti kadhaa zinaonyesha kuwa wahamiaji wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya afya kwa sababu ya hali yao ya kijamii na kiuchumi, mchakato wa uhamiaji na hali yao ya kutokuwa raia," 

Kuhusu kuandaa kampeni za chanjo, wataalam wametaka kuwe na uwazi wa kiutofautisha kati ya utekelezaji wa masuala ya uhamiaji na utoaji wa chanjo za COVID-19. 

Wameonya kwamba kampeni za umma zinazofanywa na vyombo vya Habari  zinapaswa kuweka wazi kuwa wahamiaji katika hali zisizo za kawaida hawataadhibiwa au kulengwa kwa utekelezaji wa sheria za uhamiaji wakati wanapotafuta kupata chanjo ya COVID-19. "Hakuna mtu anayepaswa kuogopa kutafuta huduma anayohitaji," 

 Walihimiza mataifa yote kuendeleza mikakati na utaratibu wa ushirikiano na msaada ili kuhakikisha upatikanaji wa chanjo ya COVID-19 kwa wote, na kuzingatia nchi ambazo zinakabiliwa na vizuizi vya kiuchumi katika kupata chanjo kwa watu wao, pamoja na wahamiaji na familia zao. 

 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter