Wanawake katika mizozo itokanayo na itikadi kali hasa wakati wa mlipuko wa COVID-19. 

7 Machi 2021

Licha ya serikali nyingi kote duniani kushirikiana katika kukabiliana na mlipuko wa COVID-19 mnano mwaka 2020, nchi nyingi na wananchi wake waliendelea kukosa usalama kutokana na vikundi vyenye itikadi kali. 

Uwepo wa vikundi vyenye itikadi kali ulichochea pengo la usawa, ikiwemo usawa wa kijinsia na kutishia juhudi za mataifa za kukabiliana na athari za COVID-19 kiuchumi na kijamii. Ulinzi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia unahitajika kwa dharura katika mkitadha huu. 

Ili kushughulikia suala hili, kuanzia tarehe 25 Mei hadi 5 Julai 2020, shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa, UN Women kwa niaba ya Kikosi kazi cha kijinsia cha Umoja wa Mataifa cha kukabiliana na ugaidi kiliandaa mkutano wa ushauri kwa njia ya kidigitali duniani ili kupata maoni ya asasi za kiraia kuhusu athari za mizozo katika masuala ya kijinsia. 

Washiriki walisema mlipuko wa COVID-19 ulichochea mapengo ya kijinsia yaliokuwepo, kuonesha haja ya kubadili mwelekeo katika mizozo yenye itikadi kali na ugaidi na kuwekeza kwenye miradi inayokuza usawa wa kijinsia na haki za binadamu katika jamii.  

Hapa kuna watetezi watano wa haki za binadamu na wanaharakati wa usawa wa kijinsia wakijadili kile jamii zao zinachohitaji na juhudi zao ya kujenga amani kati ya ukatili kwenye mizozo na COVID-19. 

Kuelimisha wanawake na vijana kupambana na ukatili nchini Nigeria. 

Fatima Askira ni kiongozi chipukizi nchini Nigeria na pia mjenzi wa amani. Alizaliwa na kukulia katika jimbo la Borno lililo ngome ya wapiganaji wa Boko Haram Kaskazini mashariki mwa Nigeria, alianzisha shirika la kiraia la maendeleo ya wanawake la Borno Women Development Initiative, BOWDI mwaka 2014. Kupitia shirika hilo hutekeleza miradi ya kuwafunza na kufuatilia wanawake na wasichana wa Nigeria wakiwemo wale waliokuwa mateka wa Boko Haram.  

Mama akiwa na watoto wake katika eneo la Monguno, Jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria (Picha ya maktaba)
OCHA
Mama akiwa na watoto wake katika eneo la Monguno, Jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria (Picha ya maktaba)

 

“Kwa muda mrefu Nigeria imekuwa nchi inayotawaliwa na wanaume pekee ambapo sasa pengo la kijinsia ni pana mno kuzibwa. Uwepo wa nafasi finyu za wanawake kwenye meza za maamuzi, kuendelea kutoshirikishwa kisiasa, na sasa hali iliyopo ya ukosefu wa miundombinu ya utawala vimeweka mazingira bora ya ukatili jambolinaloweza kushughulikwa kupitia kuelimisha na kuhamasisha wanawake wa mashinani.” anasema Fatima Askira, ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki 142 wa mashirika ya kiraia kwenye mashauriano haya ya kimataifa. 

 “Kwenye Borno Women Development Initiative, huwa tunasaidia wanawake na vijana kupata elimu na mafunzo, ambayo huwa ni magumu zaidi wakati wa mlipiko wa COVID-19. Sasa kwa kushirikiana na Malala Fund tunatekeleza mradi unaojikita katika kurejesha wasichana barubaru shuleni. Pia tunaandaa kozi ya muda mfupi kwa wanawake viongozi ili kujenga uwezo wao wa kutetea masuala ya wanawake na kupata ujuzi wa ajenda ya amani na usalama.” Askira anasema akiongeza, “kwa kuzingatia kwamba sisi kama vijana wa kike tuko kwneye msitari wa mbele kinatuma ujumbe chanya kwa jamii: ‘Tulizaliwa na kukuzwa hapa, hua tunavaa na kuongea kama vile mfanyavyo. Elimu imetupatia fursa ya kuleta mafanyikio katika jamii yenu. Ningeweza kufanya hivyohivyo kwako na watoto wako.’ Hata hivyo, ni lazima sote tuendelee kuhakikisha mataifa yanawajibika katika utekelezaji wa ajenda ya wanawake, amani na usalama.” 

Kushughulikiwa kisheria ni muhimu kwa mtu anaporejea katika maisha ya kawaida baada madhila ya kisaikolojia mzozoni nchini Ufilipino.   

Fatima Pir Allian ni Meneja wa Programu ya Nisa Ul Haqq fi Bangsamoro (Haki za Wanawake wa Bangsamoro), shirika ambalo hutoa jukwaa kwa wanawake wa Bangsamoro kutafsiri kwa uendelevu elimu ya Kislamu, haki za wanawake, na amani na masuala ya maendeleo.  

UN Women mwaka 2020 mwezi Februari, walitembelea kituo cha Polisi kinachoundwa na wanawake pekee.
UN Women/Ploy Phutpheng
UN Women mwaka 2020 mwezi Februari, walitembelea kituo cha Polisi kinachoundwa na wanawake pekee.

 

“Katika eneo la Bangsamoro (kusini mwa Ufilipino), bado tunatiwa hofu na kumbukumbu za mwaka 1974 ‘kuchomwa kwa Jolo’, makabiliano ya siku-saba kati ya serikali na vikundi vyenye itikadi kali vilivyovuruga na kusambaratisha jamii yetu. Nilikuwa na umri wa miaka mitano pekee wakati huo, lakini nilikua nikisikiliza simulizi za wazee katika jamii kuhusu maiti zilizotapakaa kwenye mitaa, harufu ya nyumba zilizochomwa moto kilio cha waliopoteza wapendanao au familia nzima. Karibu miaka 50 baadaye, kumbukumbu bado ziko hai,” anasema Fatima Pir Allian, ambaye hujikita kukuza matumizi ya mijadala kutatua masuala katika jamii. Na anaongeza akisema, “majadiliano katika jamii ni nyenzo muhimu ya kuwezesha watu waliohatarini zaidi katika jamii zetu kupaza sauti zao, kubadilishana mawazo na mawaidha kwamba safari zetu zifanane badala ya kutofautiana. Ili kutokomeza ukatili na kuzuia mizozo kutokea tena, ni lazima jamii zikumbuke yaliopita zijifunze namna ya kukabiliana na kiwewe. Kwenye Nisa Ul Haqq Fi Bangsamoro, tunawaalika wanawake na wanaume wa Bangsamoro kwa ajili ya kikombe cha 'kahawa' na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya mazungmuzo. Hua tunazingatia maagizo ya serikali ya kudhibiti COVID-19, ambayo ni pamoja na kutoa vifaa kinga kwa washiriki wote na kuhakikisha umbali kutoka mtu mmoja hadi mwingine.” 

Uponyaji mchakato mgumu na mrefu na hauwezi kukamilishwa kwa kazi za mashirika ya kiraia yaliopo pekee. Tunahitaji msaada wa taasisi za kiserikali kuhakikisha haki kisheria na ubadilishaji wa sera.  

Sitisha ukatili dhidi ya wanawake wa Wajir, Kenya 

Abdinasir Saman amekuwa akifanya kazi na shirika la Wajir Peace and Development Agency (WPDA) kwa miaka 10 iliyopita. WPDA ilianzishwa na viongozi wanawake wa kijamii katika kaunti ya Wajir, kaskazini mashariki mwa Kenya, katika miaka ya 1990, wakati eneo hilo lilikuwa linakumbana na mizozo ya kikoo.  

Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya
FAO/Ami Vitale
Wanawake wakiwa wamekaa juu ya magunia ya mchele na mahindi huko Wajir, Kenya

 

“Hivi karibuni mwili wa mwanamke ulipatikana mita 700 kitoka kituo cha polisi, alikuwa ameteswa na kunyanyaswa kingono. Leo kilipukaji cha kisasa kimelipuka kwneye mpaka. Ukosefu wa usalama na ukiukaji wa haki za binadamu yanatokea kila siki katika kaunti ya Wajir,” asema Abdinasir Saman, ambaye hufanya kazi wa wazee katika jamii kaskazini mashairki mwa Kenya.  

“Lakini ukatili dhidi ya wanawake na waschana, hasa ukatili w akingono na kijinsia vimeongezeka sanjari na ongezeko la ukatili wenye kitikadi kali. Wanawake wanalengwa na vikundi vyenye itikadi kali pamoja na vikosi vya usalama,” Abdinasir Saman anaendelea kueleza akiongeza kuwa, “kesi za ukatili wa kingono huripotiwa kwa wazee wa mitaani na kushughulikiwa katika mfumo wa kusuluhisha mizozo unaotawaliwa na wanaume ujulikanao kama ‘maslaxa’, ambao ni njia mbadala ya kusuluhisha mizozo inayotambuliwa na serikali pamoja na mashirika ya kiraia. Wanawake hawashirikishwi kwenye michakato kama hii ya kufanya maamuzi na mara nyingi haki zao hupuuzwa.” 

Shirika la Amani na Maendeleo ya Wajir (WPDA) limefanikiwa katika kampeni yake kupinga ukatili dhidi ya wanawake kupitia mfumo huu wa kitamaduni inaotawaliwa na wanaume kufanya maamuzi. Hata hivyo, “bado ni vigumu kufuatilia hali na kutekeleza sheria mpya katika maeneo na mashinani,” asema Saman. “Mpaka siku ya leo changamoto za wanawake na waschana wa Wajir zinashughulikiwa hapa, ukatili na mizozo vitaenndelea kuongezeka. Hasa wakati COVID-19 inaweka mazingira magumu zaidi kwa wanawake na wasichana, tunahitaji dhamira za kisasa na hatua endelevu kutoka kwa wadau wote walipo kuitikia changamoto hizi.” 

Wekeza katika kuimarisha utekelezaji wa jukumu la wanawake kuzuia ukatili nchini Jordan 

Samar Muhareb, Mkurugenzi  wa shirika la kurejesha demokrasia na maendeleo Uarabuni (ARDD), katika ziara yake kweye kambi ya wakimbizi ya Al Zaatari. 

ARDD ilishirikiana na UN Women katika juhudi za kuimarisha uwezo wa wanawake kutekeleza jukumu lao pamoja na asasi za kiraia zinazoongozwa na wanawake katika ujenzi wa amani. Picha: Na ARDD. 

“Alipokuwa akijadili kuhusu ongezeko la ukatili wa kiitikadi kali nchini Jordan na ulimwengu wa Uarabuni kwa ujumla, wanawake wanatazamiwa kama wathirika au wanaochangia kwenye itikadi za ukatili na ni kwa kiasi kidogo sana kuona wanajali kwamba wanawake kuchangia kuzuia ukatili huo. Kwenye shirika la kurejesha demokrasia na maendeleo Uarabuni (ARDD), tunajikita katika nafasi za wanawake ambazo hazijafuatiliwa vya kutosha kujenga amani katika jamii zao,” asema Samar Muhareb. 

“kwa msaada kutoka UN Women, tunashirikiana na washirika yasiyo ya kiserikali yanayoongozwa na wanawake kote nchini kuhakikisha kwamba wanaelewa na ‘kumiliki’  mpango wa Kitaifa wa UNSCR 1325 nchini Jordan. Moja ya ubunifu wetu kwenye kambi ya wakimbizi ya Za’atari ilishirikisha wanaume na wavulana wa Syria katika kampeni ya kutokomeza ukatili  wa kijinsia na ukosefu wa usawa ambayo ni muhimu kuhakikisha uwiano wa kijamii.” 

“Tumetoka mbali sana katika kuimarisha uelewa wetu kuhusu atahri za uaktili kwa wanawake na wasichana na jukumu lao kubwa katika kuishughulikia. Lakini njia ya kuleta babadiliko ni mbali/ndefu sana, na mlipuko usituzuie.” 

Wajibisha mataifa na yaunge mkono viongozi wa kike nchini Colombia 

Wakili wa Colombia, Lourdes Castro García ni Mratibu wa mradi wa Somos Defensores yaani ‘Sisi ni Watetezi’.  

Wanawake nchini Colombia wakipamba  mji wa Monterredondo kwa ujumbe wa amani.
UN Verification Mission in Colombia/Daniel Sandoval
Wanawake nchini Colombia wakipamba mji wa Monterredondo kwa ujumbe wa amani.

 

“Nilianza kama wakili kwenye kesi kubwa zinazohusisha ukiukaji wa haki za binadamu nchini Colombia, lakini nililazimika kukimbia nchi yangu mwaka 1994,” anaeleza Lourdes Castro García. “wakati mazunguzo ya amani yalipoanza nchini Colombia mwaka 2012, niliamua kurejea. Nilitaka kujiunga na ‘collective enthusiasm’ ili kuleta maendeleo kutokana na uzoefu wangu katika masuala ya haki za binadamu” 

Nchini Colombia, kwa muda mrefu ugaidi umekuwa nyenzo ya walio mamlakani kutawala na kukanyaga utu. Kufuatia mandamano ya kijamii mwaka 2016, serikali iliyataja mashirika yaliyoshiriki maandamano haya kuwa yameingiliwa na makundi yaliyojihami na pia yalikuwa yanahusika na vitendo vya kigaidi.  

“Unyanyapaa huu hutuathiri sote watetezi wa haki za binadamu na kuongoza vugu-vugu kama hizo hasa wanawake. Mtazamo hasi wa kijinsia umekita mizizi nchini Colombia kiasi kwamba wanawake hupambana tu kufikia nafasi za uongozi, hata pale tufikapo tunakumbana na aina nyingi za ukatili: kwa ngazi ya familia, maisha ya umma, na kadhalika. Mashambulio mengi dhidi ya wanawake watetezi wa haki za binadamu hayachunguzwi ipasavyo, kuamuliwa na vifungo kutolewa. Mashirka ya kiraia likiwemo Umoja wa Mataia yana jukumu kubwa sana la kutekeleza na ni lazima yawajibishe mataifa duniani.” Anaendelea Lourdes Castro García. 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter