Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Kyoto wapitisha azimio kukabili tishio la uhalifu na kujikwamiua vyema na COVID-19 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GUterres akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa kuhusu kuzuia uhalivu na haki ya jinai kupitia mtandao
UN/DGC
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GUterres akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa kuhusu kuzuia uhalivu na haki ya jinai kupitia mtandao

Mkutano wa Kyoto wapitisha azimio kukabili tishio la uhalifu na kujikwamiua vyema na COVID-19 

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia 

uhalifu na haki ya jinai  unaofanyika katika muundo 

mseto kutokana na vizuizi vya janga la COVID-19

Mkutano huo wa kimataifa umewaleta pamoja wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya uhalifu kutoka mashirika ya kimataifa, 
nchi wanachama, asasi za kiraia, wanazuoni, wataalam wa masuala ya sheria na haki na Umoja wa Mataifa ikiwemo ofisi ya Umoja
wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC miongoni mwa waandandaji na mwenyeji wa mkutano serikali ya Japan. 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo kwa njia ya mtandao kutoka makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini 

New York Marekani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea umuhimu wa mkutano huo kuhusu

uhalifu  katika kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati huu wa janga la kimataifa la COVID-19

"Kuzuia uhalifu, haki ya jinai na sheria vina jukumu muhimu katika kufufua tena mkataba wa kijamii kati ya nchi nawatu wake. Ajenda ya mkutano wa 14 wa  uhalifu inalenga majibu tunayohitaji ili kuimarisha kuzuia uhalifu na haki ya jinai katikamgogoro 

wa sasa. Hii ni pamoja na mikakati ya kuzuia uhalifu ili kuhimili maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hatua jumuishi ili kuimarisha hatua jumuishi ili kuimarisha mifumo ya haki ya jinai, na kufufua ushirikiano wa kimataifa na msaada wa kiufundi 

katika kuzuia na kushughulikia aina zote za uhalifu. ” 

Kwa upande wake Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Vilkan Bozkir katika taarifa yake kwenye mkutano huo amesema“Tusifanye makosaa Hatutafikia malengo ya Ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu ikiwa hatutachukua hatua juu 

ya utawala wa sheria, kuzuia uhalifu na haki ya jinai. " 

Ghada Wally , Mkurugenzi mtendaji wa UNODC akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia uhalifu na haki ya jinai
Umoja wa Mataifa
Ghada Wally , Mkurugenzi mtendaji wa UNODC akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia uhalifu na haki ya jinai

Mkutano wa Kyoto 

 Mkutano wa Kyoto umebadilishwa ili kuzingatia viwango vya kiafya na usalama huku ukiwezesha ushiriki tofauti na wa kiwango 

cha juu , na sehemu ndogo ya watu na wanashiriki moja kwa moja ndani ya ukumbi wa mikutano lakini wengi wanajiunga karibu 

kupitia mtandao katika jukwaa jipya lililotengwa na mkutano huo.  

Kati ya washiriki 5,600 wa mkutano huo washiriki 4,200 wamejiandikisha kushiriki kwa njia ya mtandao.  Hii ni pamoja na 

wawakilishi kutoka nchi wanachama 152, mashirika 37 ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali 114, wataalam  binafsi 600, taasisi kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.  

Mkurugenzi mtendaji wa UNODC Ghada Waly alipongeza juhudi za washiriki wa mkutano huo  kwa"kuandika ukurasa mpya 

katika ushirikiano wa kimataifa kwa maendeleo ya kuzuia uhalifu na haki ya jinai, kuelekea jamii zenye amani na jumuishi". 

Ameongeza kuwa wakati ulimwengu wetu unateseka katika janga hii la muda mrefu, tumeungana katika dharura ya kulinda watu 

na kutomucha mtu yeyote nyuma.  

“Tuko katika kinyang'anyiro dhidi ya wakati, kwani uhalifu wa kupangwa haujachelewa kutumia janga hili kujifaidisha, 

kuanzia kuuza chanjo za bandia, kutumia wale ambao wamepoteza uwezo wa kujimudu kimaisha, na kuelekeza fedha za 

msaada kwingineko." 

Makubaliano ya Azimio la Kyoto 

Katika azimio la Kyoto lililopitishwa leo , serikali zimekubaliana hatua madhubuti za kusongesha juhudi za kushughulikia kuzuia uhalifu, 

haki ya jinai, sheria na ushirikiano wa kimataifa.  

Wajumbe katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa wa kuhusu kuzuia uhalifu na haki ya jinai mjini Kyoto Japan
Umoja wa Mataifa
Wajumbe katika ufunguzi wa mkutano wa 14 wa Umoja wa Mataifa wa kuhusu kuzuia uhalifu na haki ya jinai mjini Kyoto Japan

Nchi wanachama zitasongesha ahadi zao mbele katika kikao cha 30 cha tume ya kuzuia uhalifu na haki ya jinai kitakachofanyika huko Vienna mnamo mwezi Mei mwaka huu. 

Mkutano wa 14 wa kuzuia uhalifu na haki ya jinai uliahirishwa na uamuzi wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutoka  tarehe yake ya awali ambayo ilikuwa Aprili 2020 kwa sababu ya janga la kimataifa la COVID-19. 

 Sherehe za ufunguzi wa mkutano huo ziilishuhudia Qatar, iliyokuwa mwenyeji wa mkutano wa 13 wa Umoja wa Mataifa kuhusu 

uhalifu uliofanyika huko Doha, akikabidhi urais wa mkutano huo kwa waziri Kamikawa wa Japan. 

Wawakilishi wawili wa jukwaa la vijana lililofanyika kabla ya mkutano huu pia waliwasilisha mapendekezo yao wakati wa kikao 

cha ngazi ya juu. 

Majadiliano yataendelea hadi Ijumaa katika mashauri rasmi na pia katika vikao vingine kadhaa vinavyofanyika kupitia mtandaoni 

na washiri wa moja kwa moja ukumbini ambayo vitashughulikia mada mbalimbali kuanzia kupambana na ufisadi kukabiliana na 

uhalifu dhidi ya wanyamapori na mtazamo wa kijinsia katika kukabiliana na ugaidi, hadi kwa athari za COVID-19 katika mazingira 

ya gerezani. 

Pia kushughulikia watoto wanaohusishwa na vikundi vya kigaidi, machafuko ya makundi yenye itikadi kali, na vijana kama 

mawakala wa mabadiliko ya kukuza utawala wa sheria.