Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia: UN yalaani shambulio la kigaidi Moghadishu

Mabaki ya gari baada ya shambulio la kigaidi Moghadishu
Picha na UN/Stuart Price
Mabaki ya gari baada ya shambulio la kigaidi Moghadishu

Somalia: UN yalaani shambulio la kigaidi Moghadishu

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea mjini Moghadishu Somalia Ijumaa 5 Machi.

Watu zaidi ya 20 waliuawa kwenye shambulio hilo lililotokea majira ya jioni saa za Moghadishu baada ya gari lililosheheni mabomu kulipuka nje ya mgahawa mmoja mjini Moghadishu zimesema duru za Habari.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo katika taifa hilo la Pembe ya Afrika.
“Katibu Mkuu kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo amesisitiza msaada na mshikamano wa Umoja wa Mataifa na wat una serikali ya Somalia wakati huu mgumu wa uhalifu huo mkubwa”.

Pi ametaka wahusika wa shambulio hilo kufikishwa mbele ya mkono wa sheria .
 "Katibu Mkuu anaamini kwamba machafuko na mashambulizi hayo hayatowakatisha tamaa watu wa Somalia katyika nia yao ya kusaka amani , utulivu na mafanikio”. Imeongeza taarifa hiyo.

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Volkan Bozkir amesema ameshitushwa san ana shambulio hilo la Moghadishu. "Ninalaani vikali shambulio hili la hila la kigaidi” amesema Bwana. Bozkir kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter Jumamosi.

Timu ya Umoja wa Msataifa nchini Somalia pia imelaani shambulio hilo lililotekelezwa na kundi la Al Shabaab.
“Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM umesema kwenye mtandao wwake wa Twitter Jumamsoi asubuhi. '
Kundi la kigaidi la Al Shabaab limekuwa likiongoza ulinzani kwa muda mrefu nchini Somalia kwa lengo la kuingangusha serikali ya nchi hiyo.
Kundi hilo lilifurushwa hadi nje ya Moghadishu mwaka 2011 na mpango wa Muungano wa afrika nchini humo AMOSOM, lakini bado linadhibiti sehemu ya taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo limekuwa katika changamoto ya utulivu kwa miaka 30 sasa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza Ku una familia ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia wametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika wa shambulio hilo na kuwatakia nafuu ya haraka wote waliojeruhiwa.