Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jeshi Myanmar acheni kuwaua na kuwafunga waandamanaji:Bachelet 

Jua likizama kwenye mji wa Yangon nchini Myanmar.
Unsplash/Alexander Schimmeck
Jua likizama kwenye mji wa Yangon nchini Myanmar.

Jeshi Myanmar acheni kuwaua na kuwafunga waandamanaji:Bachelet 

Haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelitaka jeshi la Myanmar kuacha mara moja msako wao dhidi ya waandamanaji, huku kukiwa na ripoti kwamba takribani watu 54 wameuawa tangu kufanyika mapinduzi tarehe Mosi Februari mwaka huu huku 38 kati yao wameruawa jana Jumatano pekee. 

Bi. Bachelet katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi amesema “Ni jambo la kusikitisha na kutia ghadhabu kwambna vikosi vya usalama vinawafyatulia risasi za moto watu wanaoandamana kwa amani nchi nzima. Nimesikitishwa san ana mashambulizi yaliyoorodheshwa dhidi ya watoa huduma za dharura na mafgari ya kubeba wagonjwa wakati wakijaribu kuhudumia watu waliojeruhiwa.” 

Kwa mujibu wa ofisi ya Kamisha mkuu OHCHR, kati ya watu 54 waliootrodheshwa kuuawa, takribani 30 waliuawa na vikosi vya usalama Jumatano mjini Yangon, Mandalay, Sagaing, Magway na Mon. 

Mtu mmoja aliripotiwa kuuawa Jumanne , 18 waliuawa Jumapili iliyopita na 5 kabla yah apo. 

Hata hivyo ofisi ya OHCHR inasema inasema idadi kamili ya waliouawa inaweza kuwa kubwa zaidi kwani idadi hii ni ile iliyoweza kuthibitishwa . 

Bi. Bachelet ameongeza kuwa ni vigumu kufahamu idadi kamili ya majeruhi , lakini taarifa za kuaminika zinaonyesha kwamba idadi ya chini ni mamia ya watu waliojeruhiwa katika maandamano. 

Mbali ya vifo watu zaidi ya 1,700 wamekamatwa kiholela na kuswekwa rumande kwa kushiriki katika maandamano au kujihusisha katika shughuli za kisiasa tangu jeshi la Myanmar JUNTA kushika hatamu Februari Mosi. 

Jumatano pekee kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu watu 700 walishikiliwa. 

Watu hao ni pamoja na wabunge, wanaharakati wa masuala ya kisiasa na maafisa wa uchaguzi, waandishi, watetezi wa haki za binadamu, waalimu, wahudumu wa afya, wafanyakazi wa serikali, waandishi wa Habari, viongozi wa kidini na watu mashuhuri. 

Huu ni wakati wa kubalidi mwelekeo 

 Huu ni wakati wa kufanya mapinduzi ya haki na kumaliza ukandamizaji wa kijeshi dhidi ya demokrasia-Kamishna Mkuu Michelle Bachelet 

Kamishina Mkuu pia ameelezea hiofu ya mashambulizi dhidi ya waandishi wa Habari. 

Takriban waandishi Habari 29 kuka,matwa katika siku za karibuni, na 8 kati yao wameshitakiwa kwa uhalifu ikiwemo kuchochea upinzani au chuki dhidi ya serikali au kuhudhuria mikusanyiko kinyume cha sheria. 

“Ninawataka wote wenye taarifa na ushawishi ikiwemo maafisa wa Myanmar ambao sasa wanajiunga na vuguvugu la kiraia la kutotii kuunga mono juhudi za kimataifa za kuwawajibisha viongozi wa kijeshi kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ambao unatekelezwa sasa na uliotekelezwa siku za nyuma.” Amesema Bi. Bachelet.