Wasichana zaidi ya 200 waliotekwa Nigeria waachiliwa huru:UN

2 Machi 2021

Wasichana zaidi ya 200 waliotekwa shuleni Ijumaa iliyopita huko Kaskazini Magharibi mwa Nigeria wameaachiliwa huru, hatua ambayo imekaribishwa kwa mikono miwili mashirika ya Umoja wa Mataifa na wanchi nchini humo. 

Kwa mujibu wa mratibu wa masuala ya kibinadamu na mratibu mkazi taifa Nigeria Edward Kallon , wakati hizo zikiwa ni Habari Njema, kwingine KAskazini Mashariki mwa taifa hilo la Afrika Magaribi leo raia na vituo vya misaada vimeshambuliwa , na hivyo kuendelea kudhihirisha madhila wanayoyapitia wananchi kwa miaka kadhaa ya vita na kutokuwepo kwa usalama. 

Bwana. Kallon amelaani vikali shambulio hilo kwenye eneo la Dikwa jimbo la Borno ambalo lilianza tangu jana usiku zaa za Nigeria. 

“Wakati tarifa zinaendelea kutufikia , nimesikitishwa na kukasirishwa kusikia kwamba vituo vya mashirika kadhaa ya misaada na hospital vimetriwa moto au kuharibiwa.” Amesema Kallon katika tarifa yake iliyotolewa leo Jumanne. 

© UNICEF/Apochi Owoicho
Mtoto wa kike akiwa darasani kwenye moja ya shule za msingi nchini Nigeria

Machafuko lazima yakome 

Ameongeza kuwa “Raia na wafanyakazi wa misaada , vituo vyao na mali zao havipaswi asililani kulengwa, bali vinapaswa kulindwa na kuheshimiwa  wakati wote.” 

Na ametoa wito kwa makundi yote yenye silaha kusitisha machafuko mara moja. 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa pia ameelezea hofu kubwa juu ya ulinzi na usalama wa maelfu  ya raia wa Dikwa, ikiwemo wakimbizi wa ndani wanaoishi ndani na nje ya makambi pamoja na wale ambao wamerejea katika jamii kujenga upya maisha yao baada ya kutawanywa na machafuko. 

Mji wa Dikwa ambao upo kilometa 90 kutoka mji mkuu wa jimbo Maiduguri, ni enhimu kwa ajili ya watu wanaopita kwenda sehemu mbalimbali na linatumika kama kituo cha kuelekea maeneo mengine ya Bama, Ngala, Mafa na Marte. 

Shambulio lililofanyika litaathiri msaada unatotolewa kwa watu karibu 100,000 ambao wanahitaji kwa udi na uvumba msaada wa kibinadamu na ulinzi hususan wakati huu ambapo kuna hatari ya janga la corona au COVID-19 kusambaa katika jimbo la Borno. 

Kaskazini mwa Nigeria kumekuwa katika uasi unaondeshwa na kundi la Boko Haram kwa zaidi ya muongo sasa, uasi ambao umesabnabisha maelfu kwa maelfu ya watu kutawanywa lakini pia kuongezeka kwa viwango vya njaa na utapiamlo. 

UN Photo/Eskinder Debebe
Wakimbizi kutoka Nigeria wakiwasili katika kijiji cha Goura nchini Cameroon mwezi Januari 2019

Kuachiliwa kwa wasichana waliotekwa 

Wakati huohuo leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema limefurahishwa na tarifa za kuachiliwa kwa wasicha zaidi ya 200 waliotekwa baada ya shule kushambuliwa  kwenye eeo la Jangebe, jimbo la Zamfara Kaskazini Magharibi mwa Nigeria majira ya asubuhi Ijumaa iliyopita. 

“Wakati tukisherehekea kuachiliwa kwa wasichana hawa wa shule na kutarajiwa kurejeshwa salama kwa familia zao, tunarejelea kauli yetu kwamba mashambulizi dhidi ya wanafunzi na shule sio tu ni vitendo visivyokubalika bali pia ni ukiukwaji wa haki ya mtoto kupata elimu.” Amesema mwakilishi wa UNICEF Nigeria Peter Hawkins. 

Ameongeza kuwa ni haki ambayo hakuna jamii yoyote inayopaswa kuikiuka. Bwana Hawkins ametoa wito kwa mamlaka nchini Nigeria “Kuchukua hatua zote za lazima kulinda shule nchini humo ili watoto wasiwe na hofu ya kwenda shuleni na wazazi wasiogope kuwapeleka watoto wao shuleni.” 

 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter