Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utaifa  na ubinafsi katika chanjo vinaathiri vita dhidi ya COVID-19: UN

UNICEF imeanza kusambaza mabomba ya sindano kwa ajili ya kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 duniani kote chini ya mkakati wa COVAX
© UNICEF/Charles Asamoah
UNICEF imeanza kusambaza mabomba ya sindano kwa ajili ya kampeni ya chanjo dhidi ya COVID-19 duniani kote chini ya mkakati wa COVAX

Utaifa  na ubinafsi katika chanjo vinaathiri vita dhidi ya COVID-19: UN

Haki za binadamu

Jopo la wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wametoa ombi  kwa wajumbe wa shirika la biashara duniani WTO kufikiria kuondoa masharti katika utengenezaji chanjo dhidi ya corona au COVID-19 kwa lengo la kutoa ulinzi kwa wale walio masikini kabisa duniani.