Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yawaweka kizuizini wasaka hifadhi, UNHCR yatafuta njia ya kufikia suluhu.  

Tanzania
World Bank/Hendri Lombard
Tanzania

Tanzania yawaweka kizuizini wasaka hifadhi, UNHCR yatafuta njia ya kufikia suluhu.  

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, kupitia taarifa yake iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi, limesema linasikitishwa sana na msururu wa ujumbe wa kusikitisha ambao limekuwa likipokea kutoka kwa kikundi cha waomba hifadhi 10 ambao hivi sasa wamewekwa kizuizini katika eneo la Mutukula, kaskazini magharibi mwa Tanzania.  

“Wanaotafuta hifadhi wameelezea hofu yao kwa usalama wao baada ya kufukuzwa kutoka Tanzania.” Imeeleza taarifa hiyo ya UNHCR.  

UNHCR imeendelea kutetea kwamba wakimbizi na wanaotafuta hifadhi, pamoja na wale wanaodai wanahitaji ulinzi wa kimataifa, hawawezi kurejeshwa katika nchi zao za asili hadi madai yao yatakapotathminiwa vizuri na mamlaka husika, kulingana na kanuni ya kimataifa ambayo inazuia mataifa kufukuza au kurudisha watu katika eneo ambalo maisha yao au uhuru wao vitatishiwa. 

UNHCR inaisihi Serikali ya Tanzania, ili kupata nfursa ya kuwafikia haraka wasakahifadhi hao walioko kizuizini ili kusaidia katika tathmini ya madai yao binafsi.  

Taarifa imesema, “UNHCR ina matumaini kuwa mamlaka zinazohusika nchini Tanzania zitashirikiana nasi kutatua hali hii kulingana na majukumu yao chini ya sheria za kimataifa.”