Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres apongeza Niger kwa uchaguzi huku akilaani walioua maafisa wa uchaguzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
TASS/ UN DPI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Guterres apongeza Niger kwa uchaguzi huku akilaani walioua maafisa wa uchaguzi

Haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza serikali ya Niger na wananchi wake kwa kuwezesha kufanyika kwa awamu ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo licha ya changamoto za kiusalama na kibinadamu.

Uchaguzi huo ulifanyika tarehe 21 mwezi huu wa Februari licha ya taifa hilo kugubikwa na changamoto hizo pamoja na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Katibu Mkuu Guterres amelaani hata hivyo "mauaji ya maafisa wa uchaguzi kwenye mikoa ya Tillabéri na Diffa yaliyofanyika siku ya uchaguzi. Pia amelaani mashambulio yaliyofanywa na watu wenye silaha katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo."

Guterres ametuma salamu za rambirambi kwa familia za watu waliouawa na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu Mkuu amerejelea azma ya Umoja wa Mataifa ya kuungana na serikali ya wananchi wa Niger katika juhudi zao za kusaka utulivu na maendeleo endelevu.

Uchaguzi mkuu nchini Niger ulifanyika tarehe 27 mwezi Desemba mwaka jana wa 2020 kuchagua Rais na wabunge. Hata hivyo kwa kuwa hakuna mgombea urais aliyepata kura nyingi zaidi kushika wadhifa huo, awamu ya pili ilifanyika tarehe 21 mwezi huu wa Februari,