Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sababu 6 kwa nini wanawake wana njaa zaidi kuliko wanaume

Fatema, mama wa watoto wanne, mumewe alifariki dunia nchini Myanmar na sasa yeye anaishi Bangladesh. Anafanya kazi kwenye duka la kuuza kuku na anapta dola 1.18 kwa siku.
WFP/Saikat Mojumder

Wanawake

Februari 20 ni maadhimisho ya siku ya haki ya masuala ya kijamii. Lakini tunaendelea na muongo mpya tukiwa na chini ya miaka 10 kufikia lengo la kuwepo usawa wa kijinsia. Kwa bahati mbaya bado tuna safari ndefu kwa kitu kilicho muhimu kama chakula na takribani theluthi mbili ya nchi zote duniani wanawake wako kwenye hatari zaidi ya kufa njaa. Kwa kila suala linalowabagua wanawake hufuata lingine la kuwaweka wanawake karibu na umaskini na njaa.

Hizi ni njia sita ambazo UNFPA kupitia wavuti wake imezichapisha kuonesha ni kwa vipi wanawake wana njaa ya Chakula, Usawa na Mabadiliko

Katika kila kona ya ulimwengu  wanawake wako katika nafasi kubwa ya kukumbwa na umaskini kuliko wanaume 

Mara nyingi hili hutokea kwa sababu wanawake hupata malipo kidogo au hawalipwi kabisa. Wanawake hufanya kazi mara 2.6 zaidi ya kazi wanayofanya wanaume na hulipwa asilimia 23 chini ya kiwango wanachohitaji kulipwa kwa kazi waliyofanya.Kasoro hii huonekana nyumbani kwa  sababu wakati wanawake hufanya kazi huwekeza asilimia 90 ya kipato chao kwa familia zao ikilinganishwa na wanaume ambao huwekeza tu asilimia 35.

Adut Hol anamwagilia mboga za majani katika bustani yake nchini Sudan Kusini akitumia stadi alizojifunza kutoka WFP. “Nafanya kazi kwa bidi kwa sababu hii ndio njia ya kuniwezesha kuishi,” anasema Adut.
WFP/Gabriela Vivacqua

Katika sehemu nyingi za dunia  wanawake hawaruhusiwi  kumiliki mali.

Katika baadhi ya nchi, wanawake ni mali. Licha kuwa wanawake huchukua nafasi muhimu kama wakulima na wafanyabiashara, mara nyingi wao hunyimwa haki na usaidizi ambao wanaume hupata.
Mfano mzuri ni katika kilimo: Karibu nusu ya wakulima wote wadogo ni wanawake licha ya kuwa ni asilimia 13 ya wao ndio hukumiliki mashamba wanayoyatumia. Kupunguza pengo hili inaweza kuongeza mazao kwenye mashamba yanayosimamiwa na wanawake kwa asilimia 20 au 30.
Kwa kifupi kuwapa wanawake nafaka, mbolea na vifaa yaweza kuwalisha watu kati ya milioni 100 na 150 zaidi kila mwaka.

Sheria za kibaguzi dhidi ya wanawake

Kwa mfano kwa wastani, wanawake wana robo tatu ya usalama walio nao wanaume wakati wanafanya kazi ikiwemo marufuku za ajira na sheria dhidi ya unyanyasaji wa kimapenzi. Hali hii inatajwa kuwa mbaya sana Mashariki ya Kati na Kaskaznia mwa Afrika ambako wanawake hupewa chini ya asilimia 50 ya haki wanazopata wanaume. Kwenye nchi 18 wanaume wana haki ya kuwazuia wake zao kufanya kazi.
Hakuna sheria zinazowalinda wanawake dhidi ya ghasia za nyumbani kwenye nchi 49.

Mama huyu kutoka Nigeria ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wanawake ambao tegemeo lao ni mgao wa kila mwezi wa fedha kutoka WFP wa dola 12 kwa ajili ya kulisha watoto wao.
WFP/Simon Pierre Diouf
Mama huyu kutoka Nigeria ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wanawake ambao tegemeo lao ni mgao wa kila mwezi wa fedha kutoka WFP wa dola 12 kwa ajili ya kulisha watoto wao.

Tamaduni na mila zinazobagua wanawake

Tamaduni hizi ni pamoja na ndoa za utotoni na ukeketaji wa wasichana. Tamaduni kama hizi zinaweza kuwa zenye matokeo mabaya kwa afya zao, zinaweza kukatiza masomo yao na hata kuwanyima uwezo wao na kuwalazimisha kuwategemea kabisa wanaume.
Wakati wa majanga wanawake wako kwenye hatari ya kuathiriwa na njaa na wanaweza kubaguliwa kijinsia hata kufikia misaada. Kwenye baadhi ya nchi tamaduni zinasema kuwa wanawake ndio wanakula wa mwisho baada ya wanaume wote kulishwa. 

Mume wa Deborah aliuawa siku ambayo alijifungua mtoto wao wa mwisho. Hivi sasa yeye ndiye anayetunza familia yake.
WFP/Gabriela Vivacqua
Mume wa Deborah aliuawa siku ambayo alijifungua mtoto wao wa mwisho. Hivi sasa yeye ndiye anayetunza familia yake.

Hedhi, ujauzito na kujifungua hufanya wanawake kukumbwa  na ghasia na utapimlo

Wananawake waliofikia umri wa kuzaa, theluthi moja wana upungufu wa damu hali ambayo inaweza kusababisha kushindwa kufanya kazi kwa viungo vya mwili iwapo hawatapewa matibabu.
Akina mama wanaokumbwa na utapiamlo wanaweza  kujifungua watoto walio na uzani mdogo ambao wanaweza kufa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano.
Mwaka 2015 zaidi ya wanawake 300,000 walikufa wakati wa kijifungua au kutokana na matatizo yatokanayo na ujauzito. Hii ni sawa na mwanamke moja kwa kila dakika mbili.

Sekina Hassen (kulia) na wenzake wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Udassa Repi wakinywa ui. Hupata huduma hii kila asubuhi kutokana na msaada wa WFP na hivyo wanaweza kuzingatia masomo badala ya kushinda njaa.
WFP/Kiyori Ueno

Katika elimu wavulama mara nyingi hupata msaada zaidi kuliko wasichana.

Katika jamii zinazowapendelea wavulana, wasichana wanaweza kutelekezwa, kunyimwa huduma za afya na hata kupewa chakula kidogo au chenye kiwango cha chini.
Tofauti na kupata huduma iliyopo kati ya wanaume na wanawake na elimu huwaacha wanawake katika hali duni kiuchumi na kijamii.
Utafiti mmoja uligundua kuwa elimu ya wanawake ilichangia asilimia 43 katika kupungua kwa tatizo la utapiamlo kwa watoto kwa muda fulani.
Mwaka 2017 theluthi mbili ya watu ambao hawakuwa na uwezo wa kuandika na kusoma walikuwa ni wanawake.