Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yapokea kwa furaha kurejea rasmi kwa Marekani katika Mkataba wa Paris. 

Mabadiliko ya hali ya hewa Texas yameleta dhoruba zisizo na msimu za theluji na kusababisha kuzima kwa umeme katika jimbo hilo nchini Marekani.
Unsplash/Matthew T. Rader
Mabadiliko ya hali ya hewa Texas yameleta dhoruba zisizo na msimu za theluji na kusababisha kuzima kwa umeme katika jimbo hilo nchini Marekani.

UN yapokea kwa furaha kurejea rasmi kwa Marekani katika Mkataba wa Paris. 

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, amesema "kiunganishi kilichokosekana kilidhoofisha jambo zima" akiwa anaeleza kipindi ambacho Marekani haikuwepo katika utekelezaji wa  mkataba wa Paris unaolenga kupambana na mabadiliko ya tabianchi.  

Katika mkutano uliohudhuriwa na Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani kuhusu tabianchi, John Kerry, kwa njia ya mtandao, Marekani imeendelea kuonesha utayari wa kuungana ten ana ulimwengu katika kuifanya dunia kuwa mahali salama pa kuishi wakati huu na hata kwa vizazi vijavyo. 

Marekani imethibitisha rasmi kurudi katika Makubaliano ya Paris kwenye hafla iliyofanyika Ijumaa hii katika Umoja wa Mataifa. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Rais Joe Biden kuchukua wadhifa mnamo Januari 20, na kuanzisha mchakato wa siku 30. 

Kujiondoa kwa Marekani katika mkataba, ambako kulifanyika rasmi mwaka jana 2019, kuliifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza nay a pekee kujiondoa katika makubaliano ya ulimwengu yaliyopitishwa mwaka 2015.   

Matumaini 

Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kurejea kwa Marekani katika Mkataba wa Paris kunaashiria "siku ya matumaini". Akizungumza katika kikao hicho, António Guterres amerejelea kuwa kitendo hicho ni "habari njema" kwa nchi na ulimwengu. 

Guterres pia amemkumbusha Bwana John Kerry, tukio la mwaka 2016 ambapo mjumbe huyo maalum wa Rais wa Marekani, alisaini mkataba wa huo wa Paris akiwa na mjukuu wake ili kuonesha kuwa, huo haukuwa tu mkataba wa kizazi hiki, bali pia kizazi kijacho.   

John Kerry, alipotia saini Mkataba wa Paris akiwa na mjukuu wake  katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mnamo Aprili 2016.
a VoiUN Photo/Amandsard
John Kerry, alipotia saini Mkataba wa Paris akiwa na mjukuu wake katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mnamo Aprili 2016.