Visa vipya vya ebola vimethibitishwa nchini Guinea-WHO

15 Februari 2021

Wataalamu wa afya wametangaza mlipuko wa Ebola Jumapili katika Kijiji cha Gouéké in N’Zerekore baada ya visa vitatu kuthibitishwa na maabara ya kitaifa hii ikiwa ni mara ya kwanza ya kisa kipya kuripotiwa tangu kumalizika kwa mlipuko mwaka 2016 imesema taarifa ya Shirika la afya ulimwenguni la Umoja wa Mataifa, WHO.

Kupitia taarifa yake iliyotolewa, Brazaville, Jamhuri ya Congo na Conakry, Guinea, WHO imesema uchunguzi wa awali ulithibitisha kwamba muuguzi katika kituo cha afya mashinani alifariki mnamo Januari 28, 2021 na baada ya mazishi yake watu sita waliohudhuriwa wameripotiwa kuwa na dalili zinazofanna na za Ebola na wawili kati ya hao wamefariki na wane wako hospitalini.
Guinea ni moja ya nchi tatu zilizoathiriwa vibaya kati ya mwaka 2014-2016 wakati wa mlipuko wa ebola Afrika Magharibi mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu ilipogunduliwa mwaka 1976.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Dr Matshidiso Moeti amesema, “inazua wasiwasi mkubwa kuona kulipuka kwa ebola Guinea, nchi ambayo tayari imetaabika kutokana na ugonjwa huo. Hatahivyo kwa kuzingatia ujuzi na uzoefu uliopatikana wakati wa mlipuko wa awali, timu za afya nchini Guinea wameanza kazi ya kufuatilia mwenendo wa virusi na kuzuia ueneaji.
WHO inasaisia mamlaka katika uchunugzi, ufuatiliaji na matibabu kwa ajili ya kushughulikia mlipuko huo.
Wafanyakazi wa WHO tayari wako mashinani kudhibiti ueneaji lakini pia kufikia jamii kwa ajili ya kuhakikisha ushiriki wao kukailiana na mlipuko. Aidha shirika hilo linasaidia na kupata chanjo shidi ya ebola ambayo imelkuwa na mchango mkubwa katika kuzuia mlipuko wa ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Kwa kuwa mlipuko wa ebola ni katika maeneo ya mpakani, WHO inafanya kazi na mamlaka wa afya nchini Liberia na Sierra Leone ili kuimarisha uchunguzi katika jamii mpakani na kuimarisha uwezo wa kuchunguza visa katika vituo vya afya. WHO inawasiliana na nchi zingine zilizohatarini ikiwemo to Cote d’Ivoire, Mali, Senegal na nchi zingine. 
Wakati wa mlipuko wa ebola Afrika Magharibi kulikuwa na visa 28,000 na visa 11,000. Mlipuko ulianza nchini Guinea na kuenea  mpakani na kufika Sierra Leone na Liberia.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter