Wiki hii tuna mpango wa kutuma walinda amani kote Sudan Kusini-David Shearer

11 Februari 2021

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, David Shearer, akizungumza na vyombo vya habari katika mji mkuu Juba, ameonya kuwa utekelezaji polepole wa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mnamo mwaka 2018 unaleta tishio moja kwa moja kwa amani ambayo tayari ni dhaifu katika taifa hilo jipya zaidi ulimwenguni.

Bwana Shear ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, ametaka msaada zaidi na pia kwamba walinda amani wapewe fursa ya kuzifikia jamii zenye uhitaji. Shearer anasema, “wiki hii, tuna mpango wa kupeleka walinda amani kwenye vituo saba vya muda kote nchini. Matumaini yetu makubwa ni kwamba, ikiwa tunaweza kupeleka walinda amani mapema msimu wa kiangazi, tuna nafasi nzuri ya kufanikiwa kuzuia vurugu kabla haijatokea. Hata hivyo, maeneo mengine yamekuwa magumu kufikia. Jaribio letu la kufikia Romich huko Warrap, kwa mfano, limekuwa likizuiliwa kila wakati. Kimsingi, tuna doria ambayo iko njiani hivi sasa kuelekea huko ambayo imezuiliwa kwa siku ya tano zilizopita.”  

Kuongezeka kwa mapigano kati ya jamii tofauti za kabila huko Warrap, Maban na sehemu za Jonglei kumesababisha mamia ya vifo na na kutanwanywa kwa miezi michache iliyopita. Wakati walinda amani wa UNMISS wameongeza uwepo wao na kufanya doria katika maeneo yenye hatari ya kutokea vurugu, mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kushughulikia sababu kuu za mivutano miongoni mwa jamii. 

Aidha Shearer kazi inayofanywa na UNMISS kusaidia amani ya kudumu, hususan miradi inayoendelea ya ukarabati wa barabara ya urefu wa kilomita 3,200 iliyofanywa na wahandisi wa UNMISS kutoka nchi saba tofauti. Amesema, “kuboresha barabara kunaboresha uhusiano na mawasiliano kati ya mikoa; inaongeza biashara na ajira lakini  muhimu zaidi, inaunda fursa za kupatanisha na kujenga amani. Hiyo hakika imekuwa uzoefu wetu. Kwa hivyo, kazi yetu ya uhandisi inafanya mengi kukuza amani kama juhudi nyingi za upatanisho kwa sababu wanajenga miundombinu hiyo na mtandao kati ya watu.” 

Pia Mkuu huyo wa UNMISS ameeleza kuwa ubadilishaji wa vilivyokuwa vituo vya ulinzi wa raia kuwa kambi za wakimbizi wa ndani umeenda kwa mafaniko katika maeneo ya Bor, wau na Juba na kwamba UNMISS inashirikiana na serikali ya Sudan Kusini kuhakikisha vituo viwili vilivyosalia vya Bentiu na Malakal navyo vinabadilishwa mapema hivi karibuni.  

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter