Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutumia chanjo ya AstraZeneca ni sahihi:WHO 

Mtu wa kujitolea apokea chanjo dhidi ya COVID-19 ya AstraZeneca nchini Uingereza.
University of Oxford/John Cairns
Mtu wa kujitolea apokea chanjo dhidi ya COVID-19 ya AstraZeneca nchini Uingereza.

Kutumia chanjo ya AstraZeneca ni sahihi:WHO 

Afya

Jopo la wataalam wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO wakizungumzia hofu iliyotanda kuhusu ufanisi wa chanjo AstraZenica (AZ) dhidi ya corona au COVID-19 wamesisitiza kwamba ni hatua sahihi kwa kila mtu kutumia chanjo hiyo hata katika nchi ambazo kumeibuka aina nyingine ya virusi vya corona. 

Akizungumza mjini Geneva Uswisi Jumatano mwenyekiti wa jopo la kimkakati la kundi la wataalam wa ushauri kuhusu chanjo SAGE, Dkt. Alejandro Cravioto amesema “Hata kama kuna mzunguko wa virusi tofauti nchini hakuna sababu tunayoiona sasa ya kuacha kutumia chanjo hiyo ya AstraZeneca kama inavyopaswa kwa sasa ili kuweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo miongoni mwa wanajamii.” 

Hatua ya tangazo hilo imekuja kufuatia takwimu zilizotolewa hivi karibuni kutokana na utafiti uliofanyika nchini Afrika Kusini zikionyesha kwamba chanjo ya AstraZeneca kinga yake ni ndogo dhidi ya virusi vipya vya corona miongoni mwa wazee.kt. Joachim Hombach akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari ameelezea utafiti huo kama ni wa kiwango kidogo huku Dkt. Craviota akiongeza kwamba wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65 walioshiriki kwenye utafiti huo ni wachache. 

Naye Dkt. Kaste O’Brien mkuu wa chanjo wa WHO amesema kuwa “matoikeo ya utafiti wa Afrika Kusini hayakuwa na jibu kamilifu, ingwa yalionyesha ufanisi mdogo dhidi ya ugonjwa dahifu na wa wastani.” 

Ukosefu wa takwimu 

Ameongeza kuwa kilicho muhimu zaidi ni “Kutokuwepo kwa ushahidi kwenye utafiti huo wa endapo chanjo ya AZ ina ufanisi dhidi ya ugonjwa mahtuti , waliolazwa hospitalini na kifo, na hayo ndio matokeo makubwa na yenye athari kubwa kwa uamuzi ya kutolewa kwa chanjo mapema”. 

Na kutoka kwenye utafiti hadi kwenye hatua za kukabiliana na virusi vipya kwa chanjo zilizo kwenye majaribio hadi sasa, Dkt. O’Brien ameeleza kwamba athari kubwa zaidi imekuwa miongoni mwa wagonjwa wenye afya duni.  

Katika chanjo zote kuna matokeo tofauti, matokeo makubwa zaidi ni dhidi ya ugonjwa mkali zaidi na ufanisi mdogo ni kwa ugonjwa wa wastani na kisha kwa walio na dalili ndogo na hiki si kitu cha kipekee kwa chanjo za corona. Katika chanjo zote kuna matokeo tofauti”. 

Majaribishi yanaonesha kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona ina uwezo mkubwa wa kuzuia hatariza COVID-19.
University of Oxford/John Cairns
Majaribishi yanaonesha kwamba chanjo dhidi ya virusi vya corona ina uwezo mkubwa wa kuzuia hatariza COVID-19.

Hakuna ukomo wa rika 

Chanjo inapaswa kutolewa kwa dozi mbili kwa watu wote wenye umri wa zaidi ya miaka 18 bila kuwepo na kikomo cha umri wa juu amesema Dkt. Craviota na kuongeza kuwa muda bora kati ya chanjo ya kwanza nay a pili ilikuwa ni wiki 8 hadi 12 ili kuhakikisha kinga imeongezeka mwilini . 

Ingawa chanjo ni salama, mwenyekiti wa SAGE amesema kwa sababu ya ukosefu wa takwimu bado haijawezekana kutoa pendekezo la iwapo chanjo hiyo inapaswa kutolewa kwa wanawake wote wajawazito au wanaonyeonyesha. 

“Uamuzi unapaswa kuchukuliwa baina ya mt una mt una ufanywe na daktari” amesisitiza Dkt. Cravioto. 

Na kwa sababu ya ukosefu wa chanjo  na haja ya kuendelea kudhibiti uwezekano wa virusi kusambaa zaidi ameshauri kwamba wasafiri wa kimataifa hawapaswi kupewa chanjo. 

Hakuna muda wa kupoteza 

Mwanasayansi mkuu wa WHO Dkt. Soumya Swaminathan akiongeza sauti yake katika hili amezihimiza nchi kutumia chanjo ya AstraZeneca haswa wale ambao itakuwa ni kinga yao pekee dhidi ya virusi kwani hakuna wakati wa kupoteza. 

“Nchi nyingi ambazo bado zinasubiri kuzisha chanjo na chanjo hii inaweza kuwa ni ya kwanza kwa hakika faida ni nyingi zaidi ya hatari.” 

Dkt. Swaminathan pia ametoa wito wa ufuatiliaji mkubwa wa muundo wa uambukizaji wa COVID-19 katika miakati mbalimbali ikiwemo mkakati wa afrika wa Pathogen Genomics. 

“Katika nchi nyingine hali inaweza kuwa ni kwamba kwa mpangilio mdogo sana wameweza kugundua tofauti lakini hawajui inavyoenea, hivyo wamekuwa waangalifu sana katika kufanya maamuzi kutokana na takwimu ndogo walizonazo.” 

Hadi kufikia sasa kumekuwa na wagonjwa 109,555,206 wa COVID-19 waliothibitishwa pamoja na vifo 2,333,446 vilivyoripotiwa kwa WHO. 

Wito wa mshikamano wa chanjo 

Katika suala linalohusiana na chanjo, wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa la WHO na la kuhudumia watoto UNICEF wametoa wito wa dharura wa mshikamano kwa ajili ya chanjo. 

Mkuu wa Who Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus na Henrietta Fore wamewataka viongozi “waangalie zaidi ya mipaka yao na watumie mkakati wa kimataifa wa chanjo ambao unaweza kumaliza kabisa janga la COVID-19 na kudhibiti kuzuka kwa virusi vipya.” 

Kati ya dozi milioni 128 za chanjo zilizotolewa hadi sasa , zaidi ya robotatu  ya chanjo hizo zimetolewa katika mataifa 10 tu ambayo ni tajiri wamesema wakuu hao na kuongeza kuwa “Huu ni mkakati wa kujiangamiza wenyewe kwani utagharimu Maisha ya wat una uwezo wao wa kuishi” wamesema maafisa hao wa Umoja wa Mataifa kabla ya kuonya kwamba pia utatoa nafasi kwa virusi hivyo kujibadili na kuhepa chanjo na hivyo kuathiri juhudi za kujikwamua kiuchumi na janga hilo. 

Ili utoaji wa chanjo uweze kufanyika katika nchi zote duniani katika siku 100 za kwanza za mwaka 2021 wakuu hao wa UNICEF na WHO wamesema ni muhimu kwamba wahudumu wa afya ambao wamekuwa msitari wa mbele kukabili janga hili katika nchi za kipato cha chini na cha wastan walindwe kwanza. 

Pia wametaka mkakati wa kimataifa wa kukabiliana na COVID-19 ACT ufadhiliwe kikamilifu ili kusaidia nchi zinazoendelea kupelekewa chanjo.