Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa nchi za Asia Mashariki na Pasifiki ulinusuru biashara duniani 2020- UNCTAD

Shehena za usafirishaji mizigo kwenye bandari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe
UNCTAD/Jan Hoffmann
Shehena za usafirishaji mizigo kwenye bandari katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya São Tomé na Príncipe

Uchumi wa nchi za Asia Mashariki na Pasifiki ulinusuru biashara duniani 2020- UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Bila mnepo wa uchumi wa nchi za ukanda wa Asia Mashariki na Pasifiki, kusingalikuwepo na kuibuka kwa biashara duniani mwishoni mwa mwaka uliopita wa 2020, wamesema wachambuzi wa biashara kutoka wa Umoja wa Mataifa wakati wakiwasilisha hii leo ripoti ya mwelekeo wa biashara duniani.
 

Mmoja wa wachambuzi hao Alessandro Nicita wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, iliyoandaa ripoti hiyo amesema, mchakato wa kujikwamua kibiashara haukuwa sawia na nchi nyingi bado zinasuasua.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mauzo ya biashara ya nje kutoka Asia Mashariki yaliongezeka kwa asilimia 12 kwenye robo ya mwisho ya mwaka 2020, ilhali uingizaji wa biashara kutoka nje uliongezeka kwa asilimia 5 pekee.

Matokeo hayo yanafuatia ukuaji wa takribani asilimia tatu wa biashara ya bidhaa kutoka China kwenye robo ya tatu ya mwaka ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2019, ambacho kilikuwa kwa ujumla ni mdororo kwa takribani nchi zote zenye uchumi wa juu.

Kuporomoka ndio mwelekeo

Ripoti ya UNCTAD imesema tofauti na mafanikio kwa China na nchi nyingine za Asia ya Kati, maeneo mengine yameshuhudia kuendelea kwa mwelekeo wa kuporomoka.

Nchi zilizokumbwa na mporomoko wa uchumi ni kama vile Brazil ambayo katika robo ya nne ya mwaka 2020, mauzo ya nje ya bidhaa  na huduma yaliporomoka kwa asilimia nne na 17 mtawalia, Urusi asilimia 19 na 34 mtawalia, India asilimia 5 na 8 mtawalia, Marekani asilimia 5 na 26 mtawalia.

Kwa China, mwelekeo ulikuwa ‘mdundo’ kwa kuwa nchi hiyo ilishuhudia asilimia 17 ya ongezeko la mauzo ya bidhaa nje nchi na asilimia 2 ya ongezeko kwa uuzaji wa huduma nje ya nchi.

Tweet URL

Afrika Kusini nayo ilipata ongezkeo la asilimia 15 la mauzo ya bidhaa nje ya nchi ilhali mauzo ya huduma yaliporomoka kwa asilimia 64 huku Japan na nchi za Muungano wa Ulaya zikishuhudia uuzaji wa bidhaa nje ya nchi ukiporomoka kwa asilimia tatu na biashara ya huduma ikiporomoka kwa asilimia 20 na 14 mtawalia.

Kwa ujumla ripoti hiyo imesema biashara baina ya nchi za kusini au zinazoendelea ilisalia chini  ya wastani bila kujumuisha zile za Asia Mashariki.

Sekta za nishati na usafirishaji zilisalia nyuma

Wachambuzi hao wa biashara wa Umoja wa Mataifa pia wamesema ijapokuwa sekta za uzalishaji zilikuwa na mafanikio ya kibiashara katika robo ya mwisho yam waka 2020, hali haikuwa shwari kwa sekta za nishati na usafirishaji kutokana na vizuizi vya safari vilivyosababishwa na janga la COVID-19.

Kuporomoka kwa thamani ya biashara

Kwa kumulika thamani ya biashara, janga la Corona lilisababisha thamani ya biashara kuporomoka kwa asilimia tisa mwaka 2020 ambapo biashara ya bidhaa iliporomoka kwa asilimia sita ilhali ile ya huduma kwa zaidi ya asilimia 16.

Makadirio yam waka 2021 yanadokeza kuibuka taratibu kwa mauzo ya bidhaa nje ya nchi sambamba na huduma kutokana na kuendelea kuvurugika kwa sekta ya usafirishaji,