UN iko tayari kusimama na India kufuatia maporomoko ya theluji

8 Februari 2021

Umoja wa Mataifa uko tayari kusimama na ikihitajika kuchangia katika uokoaji na juhudi za kusaidia kufuatia maporomoko ya theluji na mafuriko yalikumba maeneo ya kaskazini mwa India amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres Jumapili.

Takriban watu 14 wanaripotiwa kufa na zaidi ya 170 hawajulikani waliko baada ya theluji ya Himalaya kuporomoka katika jimbo la India la Uttarkhand Jumapili na kusababisha maji mengi, mawe na magofu. Miundombinu muhimu ikiwemo bwawa imeripotiwa kuharibiwa.

Watu 15 wanatajwa kuokolewa kufikia Jumatatu asubuhi saa za India.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akitoa salamu zake za rambi rambi kwa familia za waathirika na kwa watu na serikali ya India.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, wataalamu wanachunguza tukio hilo lililotokea maeneo ya vijijini ambapo sababu bado haijulikani.
 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter