Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO Tanzania yawezesha wakulima Kigoma kulima maharagwe yenye virutubisho 

Wakulima waliopokea mafunzo kutoka kwa FAO wakiwa wameshika zao la mikunde.
FAO Tanzania
Wakulima waliopokea mafunzo kutoka kwa FAO wakiwa wameshika zao la mikunde.

FAO Tanzania yawezesha wakulima Kigoma kulima maharagwe yenye virutubisho 

Ukuaji wa Kiuchumi

Mikunde ni zao lenye manufaa mengi yaonekanayo kila uchwao na ni kutokana na faida nyingi zitokanazo na mikunde ndio maana Umoja wa Mataifa umetangaza tarehe 10 mwezi Februari kuwa siku ya mikunde duniani. 

Mazao ya jamii ya mikunde yana nafasi kubwa katika kufanikisha malengo maendeleo endelevu, SDGs au ajenda 2030 ya Umoja wa Mataifa kutokana na manufaa yake. 

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema kuwa mikunde ikiwemo kunde zenyewe, maharagwe na choroko kutumika kama chakula chenye lishe bora katika mifumo mbalimbali, mikunde hurutubisha ardhi, hutumika kama zao la kufunika ardhi na pia mabaki ya mikunde hutumika kama chakula cha mifugo .

Tweet URL

 

Zao hili lenye lishe bora hupatikana kila kona ulimwenguni kote na yakadiriwa kuwa wanadamu wamekuwa wakilima na kula vyakula hivi kwa zaidi ya miaka 11,000 iliyopita.  

Uzalishaji wa mikunde

Kwa mujibu wa FAO, katika miaka 10 iliyopita uzalishaji wa vyakula jamii ya kunde  umekuwa ukiongezeka kati ya tani milioni 50 na 60 kila mwaka. Tanzania ni mojawapo ya nchi izalishayo mikunde ya aina mbalimbali ikiwemo kunde, choroko, dengu na maharagwe. 

Wakulima wa Kata ya Ruhita wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma hawakubaki nyuma katika kutambua siku ya mikunde ambapo kuelekea siku hiyo, wamevuna zao la maharagwe kutoka katika shamba darasa ambalo walipatiwa mafunzo na FAO chini ya mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP,  ambapo mafunzo ya mbinu bora za kilimo na Kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi yaliwawezesha wakulima hawa kuliendesha Shamba darasa la kikundi kwa kuzalisha maharage aina ya jesca yenye virutubisho asilia kama vile madini ya chuma na vitamini 

Soundcloud

Bwana John Burafisiye ambaye ni mkulima wa kikundi cha Lukundo kutoka Kata ya Ruhita Halmashauri ya mji wa Kasulu amesema Maharage aina ya jesca ni mazuri na yanapamba sana tena yana mchuzi mzito wenye virutubisho 

Mkulima huyo ni mnufaika wa mafunzo ya mbinu mbora za kilimo na pia mafunzo ya mbinu za uzalishaji mbegu za maharagwe yaliyofadhiliwa na FAO chini ya mradi wa Pamoja wa Kigoma unaoendeshwa katika Halmashauri 4 (Kasulu vijijini, Kasulu Mji, Kakonko na Kibondo) katika Mkoa wa Kigoma.