Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yakaribisha hatua za kwanza kuelekea utimizaji wa haki Sudan Kusini

Mapigano ya kikabilia yameathiri jamii Pibor mashariki mwa Sudan Kusini.
UN Photo/Isaac Billy
Mapigano ya kikabilia yameathiri jamii Pibor mashariki mwa Sudan Kusini.

UN yakaribisha hatua za kwanza kuelekea utimizaji wa haki Sudan Kusini

Haki za binadamu

Kamisheni ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini imekaribisha leo maamuzi ya serikali ya Sudan Kusini kuendelea na mchakato wa kuunda mahakama ya maridhiano na mbinu zingine za sheria kwa ajili ya kushughulikia ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa wakati wa mzozo. 

Katika hatua ya kutekeleza wajibu chini ya makubaliano ya kutatu mzozo ya mwaka 2018 nchini Sudan Kusini, mawaziri waliomba wizara ya haki na maswala ya katiba kuchua hatua zinazohitajika kwa ajili ya kuunda tume ya ukweli na maridhiano kufuatilia na kuorodhesha matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu na sababu ya mzozo nchini Sudan Kusini. 

Mahakama ya kutafiti na kushtaki watekelezaji wa ukiukaji wa haki za binadamu na sheria ya kiutu na uhalifu na mamlaka ya kufidia itakayoanzisha mfuko wa kuwafidia na kusaidia manusura wa mzozo. 

Katika tangazo la serikali ya Sudan Kusini la uamuzi huo lililotolewa Ijumaa Januari 29 “serikali hiyo ya mpito ya Umoja wa Mitaifa itaanzisha mahakama mseto ya Muungano wa Agfrika AU ili kushitaki ukiukwaji wa haki za binadamu. Tume ya ukweli, upatanisho na maridhiano , na mamlaka ya fidia na malipo ambayo itasimamia mfuko wa waathirika. “

Kutoka usemi hadi matokeo

“Baada ya miaka zaidi ya miwili ya ucheleeshwaji hatimaye serikali imechukua hatua za awali za kuanzisha hatua muhimu za mpito wa kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Sudan Kusini. Na endapo serikali ya Sudan Kusini iytahifadhi uaminifu wowote ule , maneno ya kisiasa lazima yatafsiriwe kwa matokeo yanayoonekana na ya kweli. ''Ameonya Yasmina Sooka , mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sudan Kusini. 

Ameongeza kuwa “Kikubwa zaidi serikali lazima ikamilishe michakato yote ya kuunda upya Bunge la mpito, ambalo litakuwa na wajibu wa kutunga sheria ya nfani ya kuanzisha mifumo mitatu ya hakimza binadamu na haki ya mpito chini ya mkataba wa amani wa mwaka 2018. Tume pia imetoa vigezo kwa serikali juu ya utekelezaji wa haraka wqa ahadi chini ya sura ya V. Tume hiyo imekaribisha zaidi tarifa ya mwenyekliti wa tume ya AU Moussa Faki akielezea msaada wake kwa serikali na watu wa Sudan Kusini katika harakati zao za amani na usalama.’’