Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UN alaani vikali shambulio la kigaidi Mogadishu

Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.
UN Somalia
Mojawapo ya picha kutoka maktaba ikionesha shambulio la kigaidi kwenye hoteli ya Benadir huko Mogadishu Somalia tarehe 25 Agosti mwaka 2016.

Mwakilishi wa UN alaani vikali shambulio la kigaidi Mogadishu

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa nchini Somalia umelaani vikali shambulizi la kigaidi lilofanywa Jumapili kwenye hotel ya Afrika katika mji mkuu Mogadishu na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wengine wengi kusalia majeruhi.
 

Taarifa iliyotolewa leo jijini Mogadishu, Somalia na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo James Swan imemnukuu akisema kuwa wamechukizwa na shambulio hilo kwenye eneo hilo ambalo mara nyingi hutembelewa na raia.
Kwa mujibu wa ripoti, kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab kimekiri kuhusika na shambulio hilo jumapili mchana na kisha kushikilia kwa muda mrefu hoteli hiyo kabla ya kuzidiwa nguvu baadaye na vikosi vya usalama vya Somalia.
Vyombo vya habari vinaripoti kuwa raia kadhaa waliokuwa wamekwama ndani ya hoteli waliokolewa na vikosi hivyo vya usalama vya Somalia.
Bwana Swan ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.
Somalia iliyoko kwenye pembe ya Afrika, imekuwa ikikabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kigaidi ambapo kikundi cha Al Shabaab kimekuwa kikiri kuhusika nayo.
Katika shambulio kama hilo mwezi Agosti mwaka jana wa 2020, takribani watu 17 waliuawa baada ya magaidi hayo kushambulio hoteli ya Elite, tukio ambalo lilisababisha mapigano ya saa saba kati ya Al Shabaab na vikosi vya usalama vya Somalia.
TAGS: Somalia, UNSOM