Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kushikiliwa kwa viongozi na mapinduzi ya mamlaka ni pigo kwa demokrasia Myanmar- Katibu Mkuu UN

Yangon, mji wa biashara wa Myanmar.
Unsplash/Kyle Petzer
Yangon, mji wa biashara wa Myanmar.

Kushikiliwa kwa viongozi na mapinduzi ya mamlaka ni pigo kwa demokrasia Myanmar- Katibu Mkuu UN

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelaani vikali kushikiliwa kwa viongozi wa kisiasa na maafisa wa serikali ikiwemo kiongozi mkuu wa Myanmar Aung San Suu Kyi na rais Win Myint na jeshi la nchi hiyo.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Jumapili, Katibu Mkuu,  ameelezea wasiwasi mkubw akufuatia kutangazwa kwa kupinduliwa kwa mamlaka ya bunge, rais na mahakama kwenda kwa jeshi.
Taarifa ya Katibu Mkuu imemnukuu akisema, “matokeo haya ni pigo kwa mabadiliko ya kidemokrasia nchini Myanmar.


Ongezeko la machafuko


Tukio hili limekuja saa chache kabla ya kufunguliwa rasmi kwa kikao kipya cha bunge. Siku chache kabla ya tukio hilo kumekuwa na ongezeko la uhasama kati ya serikali na jeshi baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Aung San Suu Kyi anayeongoza chama cha National League for Democracy (NLD) aliibyuka mshindi na kupata asilimia 80 ya viti katika bunge kwa mujibub wa ripoti kutoka vyombo vya habari. Hatahivyo jeshi na baadhi ya vyama vya kisiasa walipinga matoke ohayo kwa madai kwamba upigaji kura ulikuwa na makosa.

Aung San Suu Kyi  mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ
ICJ/Frank van Beek
Aung San Suu Kyi mbele ya mahakama ya kimataifa ya haki, ICJ

Heshimu chaguo la watu 


Katibu Mkuu amehimiza viongozi wa kijeshi kuheshimu matakwa ya watu wa Myanmar na kuzingatia demokrasia na kutatua tofauti zozote kwa njia ya majadiliano ya amani.
Ameongeza kwamba, “viongozi wote ni lazima wazingatie mabadiliko ya kidemokrasia Myanmar na kushirika majadiliano ya muhimu na kujizuia kutokana na ukatili na kuheshimu haki za binadamu na uhuru.”
Katibu Mkuu amehakikisha uungwaji mkono watu wa Myanmar katika kutafuta demokrasia, amani, haki za binadamu na kusimami sharia.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, kukshikiliwa kwa viongozi hao kulianza Jumatatu nchini Myanmar huku viongozi wa kisiasa wakishikiliwa Yangon na miji mingine Myanmar huku wanajeshi wakiwa mitaani na katika maeneo makubwa nchini.

Duru zinasema kwamba simu za rununu na mtandao vilikatwa katika mji mkuu wa Nai Pyi Taw na mji wa biashara Yangon.
Yaelezwa kwamba jeshi imetangaza hali ya dharura kwa mwaka mmoja kupitia televisheni inayofadhiliwa na jeshi. Aidha duru zinasema kwamba televisheni za taifa na kitaifa hazipatikani kweny mtandao.