Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu wa UN apata chanjo dhidi ya COVID-19 New York

Katibu Mkuu wa UN  António Guterres akipatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye shule mjini Bronx New York
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa UN António Guterres akipatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye shule mjini Bronx New York

Katibu Mkuu wa UN apata chanjo dhidi ya COVID-19 New York

Afya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema chanjo dhidi ya corona au COVID-19 ni muhimu ili kuhakikisha kila mtu kila mahali yuko salama dhidi ya janga hili hatari.

Guterres ameyasema hayo muda mfupi baada ya kuchomwa chanjo dhidi ya COVID-19 kwenye eneo la Brox jijini New York Marekani katika zoezi linaloendelea la kuwapa chanjo kwanza makundi ya watu walio hatarini zaidi kupata ugonjwa huo wakiwemo walio na umri wa zaidi ya miaka 65.

Kupitia ujumbe alioandika kwenye ukurasa wake wa twitter mara baada ya chanjo hiyo Guterres amesema“Nimebahatika na ninashukuru kupata dozi ya kwanza ya chanjo yangu ya COVID-19 leo. Ni lazima tufanyekazi pamoja kuhakikisha kwamba chanjo inapatikana kwa kila mytu kila mahali. Kwa janga hili hakuna aliyesalama haki pale kila mtu atakapokuwa salama.”

Katibu Mkuu wa UN  António Guterres baada ya kupatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye shule mjini Bronx New York
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa UN António Guterres baada ya kupatiwa chanjo ya COVID-19 kwenye shule mjini Bronx New York

Mwezi Desemba mwaka jana Katibu Mkuu alitangaza kwamba angefurahi kupokea chanjo hadharani na kusema kwamba "chanjo ni wajibu wa kimaadili kila mmoja wetu anatoa huduma kwa jamii na na ni muhimu kwa sababu hakutakuwa na hatari tena ya kusambaza ugonjwa huo".

Naye kamishina Penny Abeywardena kutoka ofisi ya meya wa New York inayohusika na masuala ya kimataifa akizungumza baada ya Katibu Mkuu kupata chanjo hiyo amesema“ Nimefurahi kwamba awamu ya hivi karibuni ya usambazaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 ambayo inajumuisha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 imeruhusu Katibu Mkuu Guterres kustahiki kupata chanjo yake. Nimefurahishwa pia kwamba kama walivyowakazi wenzie wengi wa New York, Katibu Mkuu aliweza kupata tarehe ya kuja kuchanjwa kwa kujisajili mtandaoni na kisha kufika kwenye moja ya shule zetu za umma hapa New York kupata chanjo yake. Hii itasaidia sana kujenga Imani kwa jamii zetu kwamba chanjo hiyo ni salama kwa wote.”