Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya jinamizi lake mauaji ya Holocust hayakumaliza chuki dhidi ya Wayahudi  

Picha katika makumbusho ya maangamizi makuu Marekani.
U.S. Holocaust Memorial Museum
Picha katika makumbusho ya maangamizi makuu Marekani.

Licha ya jinamizi lake mauaji ya Holocust hayakumaliza chuki dhidi ya Wayahudi  

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema katika kuwakumbuka waathirika milioni sita ambao ni Wayahudi na wengineo waliouawa kikatili wakati wa mauaji ya maangamizi makuu ya Holocust chini ya utawala wa Kinazi na washirika wao, inasikitrisha kwamba chuki dhidi ya Wayahudi bado inaendelea. 

Kupitia ujumbe maalum wa video wa skiku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa mauaji hayo ambayo huadhimishwa kila mwaka Januari 27, Guterres amesema ,maadhimisho ya mwaka huu yanafanyika yakighubikwa na kivuli kikubwa cha janga la corona au COVID-19, ambalo limedhihirisha ufa wa muda mrefu na mapengo ya haki katika jamii na kuchangia kuibuka tena kwa chuki dhidi ya Wayahudi na chuki dhidi ya wageni. 

Ameongeza kuwa “Mauaji ya maangamizi makuu ya Holocust ilikuwa ni kilele cha milenia mbili za ubaguzi, mashambulizi, kufukuzwa na mauaji ya Wayahudi mara kwa mara. Yanapaswa kuwa uamekomesha uhasama moja kwa moja lakini hayakufanya hivyo. Kwa bahati mbaya chuki dhidi ya Wayahudi iko hai nab ado inaendele. Ni lazima tufanye juhudi za pamoja haraka kukomesha hali hii” 

Kuzaliwa upya kwa chuki 

 

Leo hii kunaibuka watu wanaodhani weupe ni bora kuliko wengine na wanaounga mkono Unazi mamboleo, wakishawishi watu na kuwaingiza katika Imani hiyo kila kona ya dunia na kuongeza juhudi zao za kuikana historia, kupotosha na kuiandika tofauti historia hiyo ikiwemo ya mauaji ya maangamizi makuu ya Holocust. 

Katibu Mkuu ameongeza kuwa janga la COVID-19limewapa fursa mpya za kuwalenga walipo wacache kwa misingi ya dini, rangi, kabila, utaifa, mienendo yao ya kimapenzi, ulemavu na hadhi za uhamiaji. Na hii si haki na wala si sawa hivyo amesemesisitiza “Ni lazima tuchukue haraka hatua za pamoja kuwazuia kuendelea na vitendo hivyo.” 

Bwana Guterres amesema wakati dunia inafikiria kujikwamua vyema kutokana na janga la COVID-19 ni lazima kushughulikia changamoto hizi na mapengo yaliyodhihirishwa na janga hili, lakini pia kuimarisha ushirikiano kwa misingi ya utu wa pamoja. 

“Mwaka huu lazima uwe mwaka wa uponyaji. Uponyaji kutoka janga la corona na uponyaji wa jamii zetu zilizovujika ambazo chuki imemea mizizi kirahisi. Tunapowakumbuka waliokufa kwenye Holocust na kuwaenzi manusura kumbukumbu yetu bora itakuwa ni kuunda dunia yenye usawa, haki na utu kwa wote.”