Skip to main content

Kuibuka kusikotabirika na kutokuwa na usawa kunatarajiwa:soko ya ajira-ILO

Vijana wale ambao wamemaliza elimu ya juu wana uwezekano mdogo wa kuondolewa kwenye ajira kutokana na matumizi ya mashine
Vijana wale ambao wamemaliza elimu ya juu wana uwezekano mdogo wa kuondolewa kwenye ajira kutokana na matumizi ya mashine
Vijana wale ambao wamemaliza elimu ya juu wana uwezekano mdogo wa kuondolewa kwenye ajira kutokana na matumizi ya mashine

Kuibuka kusikotabirika na kutokuwa na usawa kunatarajiwa:soko ya ajira-ILO

Ukuaji wa Kiuchumi

Kuna ishara ya kuibuka katika soko la ajira kufuatia kusambaratishwa kwa sekta hiyo mwaka 2020 kwa sababu ya janga la ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kazi duniani, ILO. 

Makadirio ya toleo la saba ya kufuatilia mienendo ya ILO:COVID-19 na dunia ya ajira yanaashiria athari kubwa katika soko la ajira mwaka 2020. Takwimu za hivi majuzi zinaonesha kwamba asilimia 8.8 ya saaa za kufanya kazi zilipotezwa mwaka jana ikilinganishwa na robo ya nne ya mwaka 2019 ambayo ni sawa na ajira milioni 255 za saa kamilifu. Idadi hii ni takriban mara nne zaidi ya idadi iliyopotezwa mwaka 2009 wakati wa janga la kiuchumi la dunia. 

Saa hizo zilizopotezwa ni au kufuatia kupungua kwa saa anazofanya mtu kazi au upotezaji wa ajira usiotabirika ulioathiri watu milioni 114. 

Athari kwa makundi na sekta 

Wanawake wameathirika zaidi ya wanaume na janga la COVID-19 ktika kusambaratishwa kwa soko la ajira,duniani, idadi ya wanawake waliopoteza ajira ni asilimia 5 ikilinganishwa na asilimi 3.9 miongoni mwa wanaume. Wanawake hususan wana uwezekano mkubwa wa kutoka kwenye soko la ajira. 

Halikadhalika wafanyakazi vijana wameathirika na kupoteza ajira kwa kutoka kwenye soko hilo au kuchelewa kuingia huku idadi ya vijana kati ya umri 15-24 waliopoteza ajira ni 8.7 ikilinganishwa na asilimia 3.7 ya watu wazima na ni ishara ya kizazi kilichopotea imesema ripoti. 

Ripoti inaonesha athari tofauti kwa watu tofauti kulingana na hali yao ya kiuchumi na maeneo waliko huku ikiashiria kwamba sekata zilizoathirika pakubwa zitasalia nyuma wakati wakuibuka na kuongeza ukosefu wa usawa iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa. 

Sekta zilizoathirika san ani sekta ya makazi na chakula ambako ajira ilipungua kwa asilimia 20 kwa wastani ikifuatiwa na reja reja na uzalishaji tofauti na ajira kwenye sekta ya habari na mawasiliano na fedha na bima iliongezeka katika robo ya pili na tatu mwaka 2020. Aidha kulikuwa na ongezeko katika sekta ya uchumbaji migodi, mawe na bidhaa.



Kuelekea siku zijazo 

Licha ya kwamba kuna kiwango kikubwa ya kutotabirika, makadirio ya hivi majuzi yanaonesha kwamba nchi nyingi zitashuhudia kuibuka katika viwango vya juu katikati yam waka wakati programu ya chanjo ikizaa matunda. 

Ripoti inaorodhesha taswira tatu za kuibuka ; ambapo ya kwanza inazingatia makadirio ya shirika la fedha duniani ambayo inasema kuanzia Oktoba 2020 kutakuwa na kupoteza asilimia 3 ya saa za kazi duniani mwaka 2021 ambayo ni sawa na ajira milioni 90. Taswira ya tatu inakadiria usambazaji chanjo kwa kasi ndogo kutasababisha saa za kazi kupungwa kwa asilimia 4.6 wakati taswira ya tatu inaonesha kupungua kwa asilimia 1.3 kufuatia udhibiti wa janga na ongezeko la Imani ya watumiaji na biashara. 

Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Ryder amesema, “ishara za kuibuka tunazoshuhudia zinatia matumaini lakini ni dhaifu na hazitabiriki kwa kiasi kikubwa na ni lazima tukumbuke kwamba hakuna nchi moja au kundi moja ambalo linaweza kuibuka pekee yake.”