Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC yatimiza miaka 75: UN

Munir Akram, Rais wa Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC
UN/Ingrid Kasper
Munir Akram, Rais wa Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC

ECOSOC yatimiza miaka 75: UN

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limetuimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake huku dunia na Umoja wa Mataifa wakikabiliwa na changamoto kubwa zaidi za kiuchumi na kijamii na hasa mgogoro wa kiafya wa janga la corona au COVID-19 kuwahi kushuhudiwa.

ECOSOC ni moja ya vyombo vya Umoja wa Mataifa ambacho kina jukumu na wajibu wa kubabiliana na changamoto hizo amesema Rais wa baraza hilo Munir Akram katika maadhimisho ya chombo hicho hii leo Jumamosi.

Katika taarifa yake maalum ya maadhimisho haya Bwana Akram amesema“Hebu na tufanye kazi pamoja kutimiza majukumu ya ECOSOC ambayo ni moja ya nguzo kuu sita za Umoja wa Mataifa na uwezekano wa kukabiliana na changamoto hizi kubwa zaidi zinazoikabili duniani.”

ECOSOC 101

ECOSOC ni kitovu cha mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kusongesha mbele pande kuu tatu za maendeleo endelevu ambazo kiuchumi, kijamii na mazingira.

Ni jukwaa kuu la kuchagiza mijadala na fikra za ubunifu, kusaka muafaka na ushirikiano katika njia za kusonga mbele juhudi za pamoja ili kufikia malengo ya kimataifa ambayo dunia imekubaliana. Pi combo hiki kinahusika na kufuatilia mikutano mikubwa ya Umoja wa Mataifa.

Bwana. Akram ameelezea kwamba jukumu kubwa la baraza hilo chini ya katiba ya Umoja wa Mataifa ni kuchagiza viwango bora vya Maisha kwa uhuru mkubwa kupitia ushirikiano wa kimataifa.

Leo hii mashirika ya kimataifa 20, tume za kikanda na vyombo huru vinaripoti kwa baraza la ECOSOC kila mwaka.

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs
UN SDGs
Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs

Mabadiliko na malengo ya SDGs

“Kwa miaka mingi ECOSOC imekuwa ndio chombo kikuu kwa ajili ya majadiliano ya kimataifa ya kiuchumi, kijamii na sera za maendeleo”ameongeza Akram huku akisema baadhi ya mipango mikubwa ya malengo ya maendeleo asilimi 0.7 (ODA), malengo ya haki zinazokwenda sanjari na maendeleo, jinsi nchi zilizoendelea zinavyotendewa katika biashara ya kimataifa yote hayo yanajadiliwa katika baraza la kiuchumi na kijamii.

Zaidi ya hapo ECOSOC ilikuwa chachu katika kupitishwa kwa mikakati na malengo muhimu ya kimataifa ya maendeleo , mathalani malengo ya maendeleo ya milenia (MDGs) na ajenda muhimu ya 2030 kwa ajili ya maendeleo na malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs).

Kupambana na COVID-19 na maendeleo kwa wote

“Leo hii dunia inakabiliwa na changamoto kubwa kabisa ya kimataifa ya kiafya na kiuchumi tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na kuunda kwa ECOSOC “amesema Akram ambaye hivi sasa pia ndiye balozi wa kudumu wa Pakistan kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York.

Amesisitiza kwamba umasikini umeongezeka kama ilivyokuwa kwa njaa. Rasilimali fedha zinazohitajika kwa ajili ya kujikwamua kwa nchi zinazoendelea bado zinahitajika kuchangishwa.

Ufikiaji wa malengo ya SDGs bado uko njiapanda na tishio la mabadiliko ya tabianchi halikwepeki.

“Na hakuna hakikisho kwamba chanjo ya kukomesha janga la COVID-19 itapatikana kwa usawa katika nchi masikini. ECOSOC ina jukumu na wajibu wa kuchukua hatua kukabiliana na changamoto hizi.”

Akram ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutumia fursa itakayotolewa kwenye mikutano mbalimbali ya ECOSOC katika mwaka ujao kuandaa hatua za kimataifa na njia iliyo na usawa ya kusonga mbele ikiwemo kongamano la ufadhili kwa ajili ya maendeleo mwezi Aprili, jukwaa la ushirikiano wa maendfeleo na jukwaa la ngazi ya juu mwezi Julai.