Idadi ya wakimbizi wa ndani Sahel ni milioni 2, UNHCR yatoa wito kusaidia wakimbizi na jamii zinazowahifadhi

22 Januari 2021

Shirika la Umoja wa Matiafa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linatoa wito kusitishwa kwa ukatili unaoendelea katika ukanda wa Sahel ambao umesabaibsha watu takriban milioni mbili kuwa wakimbizi wa ndani. 

Ukanda wa Sahel unajumuisha nchi za Chad, Burkina Faso, Mali na Niger na una nchi masikini zaidi duniani huku wanaohifadhi jamii hizi wakifzidiwa pomoni. 

UNHCR kupitia msemaji wake Boris Cheshirkov imewambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi  hii leo kwamaba mahitaji katika ukanda huo yanaongezeka kufuatia mzozo wa vikundi vilivyojihami, umasikini uliokithiri, ukosefu wa uhakika wa chakula, mabadiliko ya tabianchi na janga la COVID-19 

UNHCR inasema kuna tishio la ukata na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza juhudi marafudi kwa ajili ya kusaidia ukanda huo. 

Idadi ya wakimbizi wa ndani katika ukanda huo imeongezeka kwa mara nne katika kipindi cha miaka minne ambapo mwanzoni mwa mwaka 2019 kulikuwa na wakimbizi wa ndani 490,000 wengi wakiwa ni kutoka Burkina Faso. 

Licha ya ukarimu ya wanaowahifadhi wengi wa wakimbzi wa ndani wanakosa mahitaji muhimu ikiwemo malazi na wanalala nje. Aidha wana mahitaji ya dharura ya makazi, maji na mahitaji ya dharura pamoja na huduma ya afya na ya kujisafi ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19. 

UNHCR kwa sasa kwa kushirikiana na wadau wanawasilisha mahitaji ya dhaura kwa maelfu waliofurushwa na wahifadhi wao. Pia wanafanya kazi kuzuia na kukabiliana na matukio ya ukatili wa kingono ambao umeenea.  

Halikadhalika wanakarabati shule na madarasa na kuunga mkono fursa za masomo kupitia mtandao. 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter