Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutangaza Houthi kuwa ni shirika la kigaidi kutakuwa na athari za kisiasa na kibinadamu Yemen:UN

Kutoka Maktaba: Meli ikitiananga kwenye bandari ya Hudaydah Yemen ikiwa imeshehemi misaada ya kibinadamu iliyotumwa na UNICEF, 30 June 2018
© UNICEF
Kutoka Maktaba: Meli ikitiananga kwenye bandari ya Hudaydah Yemen ikiwa imeshehemi misaada ya kibinadamu iliyotumwa na UNICEF, 30 June 2018

Kutangaza Houthi kuwa ni shirika la kigaidi kutakuwa na athari za kisiasa na kibinadamu Yemen:UN

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu tangazo lililotolewa leo na Marekani la kulitangaza kundi la Houthi nchini Yemen kuwa ni shirika la kigaidi, ili kutathimini athari zinazoweza kujitokeza na tangazo hilo.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo mjini New York Marekani na msemaji wake wakati wa mkutano na waandishi wa Habari, Antonio Guterres amesema“Uamuzi huo una uwezekano wa kuleta athari mbaya za kibinadamu na kisiasa.”

Taarifa yake imeongeza kuwa Yemeni inaingiza karibnu chakula chake chote kupitia uingizaji wa kibiashara hivyoTunahofia kwamba kutangazwa huko kunaweza kuleta athari mbaya ikiwemo kwa uingizaji wa chakula unaofanywa na wafanyabiashara lakini pia uingizaji wa bidhaa zingine muhimu wakati huu ambao Wayemen wengi wanakabiliwa na njaa. Operesheni za kibinadamu ambazo ni kubwa zaidi nchini humo haziwezi kuchukua nafasi ya sekta binafsi au kufidia uingizaji mkubwa wa kibiashara wa chakula na bidhaa nyingine muhimu nchini humo.”

Hatari ya baa la njaa Yemen

Taarifa hiyo ya Katibu Mkuu imesisitiza kwamba hatari inayoongezeka ya ya baa la njaa Yemen inasisitiza umuhimu kwa Marekani kutoa haraka leseni na misamaha ili kuhakikisha kuwa misaada ya kibinadamu inayofuata kanuni inaweza kuendelea kuwafikia watu wote wanaoihitaji bila usumbufu.

Kwa kuzingatia umuhimu wa uingizwaji wa kibiashara wa chakula kwa mamilioni ya uhai wa watu wa Yemen, leseni hizi na misamaha lazima vihakikishe kuwa sekta binafsi zinaweza kuendelea kufanya kazi ili kuzuia kuporomoka kabisa kwa uchumi wa taifa hilo na baa kubwa la njaa.

Pia Katibu Mkuu amesema“Tunatiwa hofu kwamba tangazo hilo dhidi ya Hoiuthi linaweza kuwa na athari mbaya kwenye hjuhudi za kuanza tena mchakato wa kisiasa nchini Yemen na pia kudumaza hata zaidi misimamo ya wahusika kwenye mzozo wa nchi hiyo. Licha ya athari za kisiasa tutaendelea kushirikiana na pande zote kuanza ten ana kuendelea na mchakato jumuishi wa pamoja wa kisiasa kufikia suluhu kamili ya mazungumzo kwa lengo la kumaliza kabisa mzozo nchini humo.”