UNICEF yalaani mashambulizi dhidi ya raia ikiwemo watoto Niger

Nchini Niger, mashambulio dhidi ya raia na vikundi visivyo vya serikali na operesheni za kijeshi zimekuwa zikiongezeka, na kufungwa kwa mipaka na hatua zingine za kuzuia COVID-19 zimesababisha maalum yaliyoko hatarini kuathirika.
© UNICEF/Juan Haro
Nchini Niger, mashambulio dhidi ya raia na vikundi visivyo vya serikali na operesheni za kijeshi zimekuwa zikiongezeka, na kufungwa kwa mipaka na hatua zingine za kuzuia COVID-19 zimesababisha maalum yaliyoko hatarini kuathirika.

UNICEF yalaani mashambulizi dhidi ya raia ikiwemo watoto Niger

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeelezea kusikitishwa na mashambulizi ya Jumamosi yaliyotekelezwa na makundi yaliyojihami dhidi ya raia kwenye vijiji vya Tchoma Bangou na Zaroumadareye,nchini Niger karibu na mpaka na Mali. 

Duru zinasema kwamba takriban watu mia moja wameuwawa ikiwemo watoto 17. 

Taarifa ya UNICEF kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dakar, Senegal na New York, Marekani inasema kwamba taarifa zisizothibitishwa zinaonesha kwamba watoto wote waliopoteza masiha, wavulana kumi na wasichana saba walikuwa chini ya umri wa miaka 16, na inadaiwa kwamba wengine waliteketezwa moto.
Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, Bi. Henrietta Fore amesema, “idadi isiyojulikana ya watoto mansura wa shambulio walipata majeraha makubwa, huku wengine wengi wamelazimika kuhama makwao. Karibu watoto 11 wametenganishwa na familia zao.”
Shambulio hili linafuaia linguine lililofanyika mnamo Desemba Toumour nchini Niger kwenye eneo la Diffa ambapo watu 45 ikiwemo watoto 10 waliuwawa. Shambulio hilo liliharibu hifadhi ya chakula, miundombinu ya maji na darasa mbili na kuathiri watu takriban 21,000. 

Bi. Fore amesema, “ukatili ambao unapuuza maisha ya watoto na familia unapaswa kulaaniwa vikali. Vitendo hivyo vya kikatili ni ukiukaji wa haki za watoto na haki za kimataifa na haki za binadamu. UNICEF inatoa wito kwa kusitishwa kwa mashambulizi dhidi ya watoto, familia zao na jamii.” 

Aidha UNICEF imesema, “pia tunaelezea rambi rambi za dhati kwa familia za wahanga na kuelezea mshikamano wa UNICEF kwa ajili ya watoto na familia nchini Niger.” 

UNICEF iko tayari kusaidia serikali ya Niger katika kusaidia manusura na familia zilizoathirika na kulinda haki za watoto  wote.